Nchemba: Marufuku wagonjwa kuchajiwa hela ya mafuta


Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwingulu L. Nchemba, amekabidhi gari la kubebea wagonjwa ambalo limetolewa na Serikali kupitia Wizara ya Afya, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kituo cha afya cha Ndago kilichopo Wilayani Iramba.

Aidha, amesema kuwa ni marufuku wagonjwa kuombwa kuchangia mafuta ya ambulance hiyo au gharama yoyote ile na kuwataka wagonjwa kutumia gari hilo bure bila kuchajiwa gharama yeyote.

“Gari hilo lipatikane kituoni wakati wote, liwe na mafuta ya kutosha na dereva awepo. Gari hili ambalo ni la kisasa litunzwe na kulindwa ili liweze kutumika kwa miaka mingi ijayo”, amesema Mwigulu.

Hata hivyo, Mwigulu ameishukuru Serikali ya awamu ya tano chini ya rais Magufuli na waziri Ummy kwa msaada huo ambao utaokoa wapiga kura wake na wananchi kwa ujumla.

Chapisha Maoni

0 Maoni