Mbunge
wa Nzega Mjini, Hussein Bashe (CCM) amefunguka na kusema kuwa kwa
twakimu mbalimbali ambazo zinatolewa na BoT zinaonyesha mambo hayapo
sawa hivyo kuna haja kubwa kwa Serikali kupitia Waziri wa Fedha kubadili
sera zake za kibajeti.
Bashe
alisema hayo akiwa Bungeni na kudai takwimu mbalimbali kutoka Benki Kuu
ya Tanzania (BoT) mwaka 2011 mpaka Disemba 2017 zinaonyesha kuwa kuna
mabadiliko makubwa na vitu kushuka kwa kasi kubwa.
"Umefika
wakati kama nchi hasa Wizara yetu ya Fedha kukubali kubadili sera zake
za kibajeti, nitatoa takwimu chache ambazo ukitazama takwimu hizi
zinazoonekana kwenye taarifa za BoT kuanzia mwaka 2011 mpaka 2017,
mzunguko wa fedha umeshuka kutoka asilimia 22% ya mwaka 211 mpaka
asilimia 1.8% ya sasa hivi, ukiangalia export hasa ya mazao ya kilimo
ambayo ndiyo yameajiri asilimia 70 Tanzania, ukichukua zao la Kahawa
mwaka 2011 gross late yake ilikuwa asilimia 55% lakini sasa hivi ni
asilimia -5.4, Cotton mwaka 2012 ilikuwa kwa asilimia 16% saizi imekuwa
kwa asilimia - 3.8%, Sisal ndiyo imekuwa na ongezeko la asilimia 2.9
iliyokuwa mwaka 2012 saizi ipo kwa asilimia 4% .
"Manufacturing
mwaka 2011 ilikuwa kwa asilimia 96% gross late sasa hivi imekuwa kwa
asilimia -244, tafsiri yake ni ndogo tu sera zetu hazichochei ukuaji wa
biashara na uchumi katika nchi.
"Takwimu
zinaonyesha Watanzania tunakuwa kwa wastani wa asilimia 2% na kitu
lakini ukuajia wetu wa kilimo ni asilimia 0.4% hakuna uwiano hapa hili
ni jambo ambalo hata tukasema humu dani ya Bunge lisifurahishe upande wa
Serikali kwa kauli zetu lakini tunajukumu la kusema ukweli na ni muhimu
kabisa Wizara ya Fedha ikakubali kwamba sera za kibajeti za Wizara ya
Fedha siyo rafiki katika kuchochea kukuza uchumi wetu" alisema Bashe
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA