Mbunge wa jimbo la Hai na Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Mhe. Freeman
Mbowe, ameongozana na Wakaguzi wa shule wa Kanda Mkoani Kilimanjaro na
Afisa Elimu Wilaya ya Hai na Diwani wa Machame Mashariki kukagua bweni
la shule ya Sekondari ya Harambee iliyopo Machame wilayani Hai Mkoani
Kilimanjaro.
Bweni hilo la kisasa lilojengwa kwa jitihada za Mbunge wa Hai kwa
kushirikiana na Diwani na wadau mbalimbali wa Elimu kutoka Mkoa wa
Kilimanjaro, lina ghorofa mbili huku likiwa na uwezo wa kuchukua
wanafunzi 181 kwa wakati mmoja.
Wanafunzi wenye sifa za kuendelea na kidato cha V na VI lakini walikosa
nafasi wataandikishwa na kuendelea na masomo katika shule ya Harambee,
sera ya Serikali inataka ili shule iwe na sifa ya kuwa na kidato cha V
na VI lazima iwe na bweni.
Elimu ni kitu muhimu, wakati wa sasa bila kuwapatia watoto elimu bora,
na kuandaa mazingira bora ya kuwapatia elimu, ni wazi tunawaandalia
wakati mgumu katika maisha yao siku za mbele, jamii haina budi
kuhakikisha watoto wanapata elimu, kila mmoja ashiriki kuhakikisha elimu
inapatikana, kila Mwenye nafasi fulani ajitahidi kuhakikisha watoto
wanapata elimu.
Tukiwa na Taifa lenye wasomi wa kutosha uzalishaji wa bidhaa zilizo bora
utakuwepo, uchumi utakuwa kwa wastani unayostahili, kila mmoja akipata
kipato kichafanya ajiletee maendeleo yake na jamii kwa ujumla.
Kila mtu atoe kipaumbele katika elimu, 1. Iwe elimu, 2. Iwe elimu na 3.
Iwe elimu, elimu kwanza kwa Taifa lenye ustawi thabiti na Imara.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA