Mbowe: Pato la Taifa limeshuka, makusanyo ya kodi yako chini na waziri amekiri hili

Image result for freeman mbowe
ANAANDIKA KAMANDA MBOWE KWENYE UKURASA WAKE WA INSTAGRAM:

Waziri wa Fedha amewasilisha mpango wa bajeti kwa mwaka ujao wa fedha, mapendekezo ya mpango wa fedha na ukomo wa bajeti, mambo machache ya msingi tumeweza kuyabaini katika hatua ya awali kwa sababu inahitaji uchambuzi wa kina zaidi.

Kwanza deni la Taifa limeendelea kukua kwa kasi sana na Waziri amesisitiza kwamba deni linalipika kwa hiyo tunaweza kuendelea kukopa, lakini ni hatari sana kwa sababu ukija kuangalia mwisho wa siku tunatumia fedha nyingi sana za ndani kulipa madeni haya na hii inaathiri bajeti ya Serikali.

Lakini dhahiri vile vile kwa takwimu zilizotolewa jana makusanyo ya kodi kwa nchi yamepungua na Waziri amekiri mwenyewe kwamba tunakusanya wastani wa trilioni moja kwa mwezi.

Hiki ni kiwango kidogo, kukusanya trilioni moja kwa mwezi ina maana inaweza kuwa Bilioni mia tisa au inaweza ikaenda hadi trilioni moja nukta kadhaa, kwa hiyo ina maana mwaka jana tulikuwa tunakusanya wastani wa trilioni nukta mbili sasa ni wastani wa trilioni moja, kwamba ina maana kuna kupungua kwa mapato yatokanayo na kodi yanayokusanywa na Taifa.

Jambo moja ambalo nafikiri ni jema kwenye bajeti hii Serikali haikuongeza sana matumizi unaweza kuona kwamba imeongeza matumizi kutoka bajeti ya mwaka jana kwa Shilingi Bilioni mia saba na arobaini na kitu.

Tofauti na mwaka jana ambako waliongeza bajeti kwa zaidi ya trilioni tano, jambo ambalo vile vile walishindwa kuzikusanya zile, Kwa hiyo ni vyema Serikali ikajikita kwenye hali halisi ya mapato halisi ambayo wao wanayapata kuliko kujaribu tu kupanua bajeti ionekane kubwa wakati hawawezi kukusanya mapato yale.

Kwa kitendo cha safari hii Serikali kuongeza bajeti kwa Shilingi pungufu ya trilioni moja ni ishara kwamba wametambua kwamba makusanyo hayawi rahisi kama walivyofikikiria wao mwanzoni.


  • Kwa kitendo cha safari hii Serikali kuongeza bajeti kwa Shilingi pungufu ya trilioni moja ni ishara kwamba wametambua kwamba makusanyo hayawi rahisi kama walivyofikikiria wao mwanzoni.

    Lakini niseme tu bado tujaona msukumo wa kutosha kwenye kilimo na hii bajeti kama ilivyo bado itashindwa kuondoa umasikini hapajaonekana msukumo wa kutosha (Seriousness) wa Serikali katika suala la kilimo, hata kinachoitwa mipango ya miradi ya kielelezo bado kilimo hakipo kwenye miradi ya kielelezo na kilimo kinawahudumia wananchi walio wengi, Serikali haijaonekana kuwa serious ndio sababu mnaweza kuona sababu kwamba kilimo kimekuwa kwa asilimia tatu nukta tatu tu (3.3%) lakini kinakuwa kwa asilimia tatu nukta wakati kinawahudumia watu asilimia sabini hadi themani (70% - 80%) ya Watanzania.

    Bado hatujataka kuwekeza seriously kwenye kilimo na hili ni tatizo kubwa ambalo halitatoa jibu kwa umasikini wa Watanzania kwa sababu bado hatujaona kipaumbele chetu ni nini, sawa tutajenga miundombinu, tutajenga reli ya Standard gauge mwisho wa siku maisha ya wananchi ni jambo la msingi kweli, nakupigania maisha ya Watanzania wetu ni lazima tuweke mikakati ya kiuchumi ambayo inalenga kunyanyua sekta kilimo, ufugaji na uvuvi kwa sababu hizi sekta tatu zinawaguza Watanzania walio wengi, bado vipaumbele vya Serikali yetu katika eneo hili bado halijaguswa vya kutosha.

Chapisha Maoni

0 Maoni