JPM atajwa kuwania tuzo za FORBES


Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania atajwa kuwania, kati ya watu muhimu wa Afrika, tuzo za FORBES mwaka 2016. Mtandao wa Forbes huendesha shindano hili kila mwaka na mwaka huu JPM ametajwa kama mshiriki kati ya wengine watano barani Afrika akiwa kama kiongozi ambaye amesaidia kuinua uchumi wa nchi ndani ya muda mchache wa utawala.

Wengine waliotajwa ni pamoja na Michiele Le Roux ambaye anatajwa kuwa mwanzilishi wa benki ya Capitec ambayo ilienea sana kwa waafrika kusini. Mwingine ni mwanamama Thuli Madonsela ambaye ni mwana ulinzi wa umma nchini Afrika kusini ambaye, licha ya kutishiwa kuuawa hakukata tamaa kufanya kazi yake. Ameenah Ghurib, rais wa Mauritania pia ametajwa kama mpiganaji mwanamazingira ambaye amekuwa akiipigania nchi yake kutokana na uharibifu wa mazingira. Watu wa Rwanda pia wametajwa kwenye kinyang'anyiro hicho kama wapambanaji wa usawa wa kijinsia nchini humo.

Waweza kushiriki kumpigia kura rais JPM hapa ili kumfanya apate kura nyingi.

Chapisha Maoni

0 Maoni