LOWASA AENDELEA KUITESA SERIKALI YA JPM.

Mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA na aliyekuwa mgombea urais tiketi ya chadema Edward Lowasa amesema kuwa serikali imepoteza mwelekeo sababu ni matatizo mengi yanayotengenezwa na serikali hii pamoja na tatizo la kuwasumbua watumishi wa umma kwa kisingizio cha uhakiki lakini serikali haina pesa za kulipa sitahiki za wafanyakazi na kutoa ajira mpya.


 Mhe.Lowasa pia alisema serikali imekuwa ya kwanza kuvunja sheria za utunishi wa umma ikiwa ni kuwasitishia ajira vijana zaidi ya 3000 walioajiriwa june 2016 bila kuwa na kosa. Alisema serikali ndiyo chombo cha kusimamia sheria ila anashangazwa na viongozi kushindwa kuheshimu sheria za nchi.

Chapisha Maoni

0 Maoni