Mafunzo Kwa Majaji mahakama ya mafisadi yakamilika!

Mafunzo ya majaji katika kuendesha Mahakama ya Mafisadi yakiwamo ya kanuni za uendeshaji yamekamilika, huku muda wa kusikiliza na kukamilisha mashauri ukiwa usiozidi miezi tisa.

Akizungumza wakati wa kikao kati ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa mjini hapa, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, (Utumishi na Utawala Bora), Angella Kairuki amesema Jaji Mkuu ameshamaliza kuandaa kanuni na majaji wameshapewa mafunzo.

Chapisha Maoni

0 Maoni