MAJALIWA: Serikali imejipanga kumaliza malimbikizo yote kwa watumishi wa umma.

Waziri mkuu wa jamhuri ya muungano ya Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amesema, serikali imejipanga kulipa malimbikizo yote kwa watumishi wa umma. Majaliwa amesema hayo akifunga sherehe za miaka 55 ya chuo kikuu cha Dar Es Salaam.

Sanjari na hilo pia, waziri mkuu amesema, serikali yake imejipanga kuhakikisha inamaliza tatizo la ucheleweshwaji mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu kuanzia mwaka huu wa masomo.

Chapisha Maoni

0 Maoni