Ndege yawaka moto kabla ya kutua nchini Marekani.

Ndege ya shirika la ndege la America Airline Flight 383, boeing 767, imeshika moto kabla ya kutua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa O'Hare jimbo la Chicago, siku ya ijumaa.


Chanzo cha moto huo inasemekana ni hitilafu ya injini. Ndege hiyo ilikuwa na jumla ya abiria 161 na wafanyakazi 9, kwa bahati nzuri wote walifanikiwa kutolewa na hakuna majeraha makubwa yaliyojitokeza.

"Reuters"

Chapisha Maoni

0 Maoni