Mashindano Miss Tanzania 2016; Diana Edward awatoa kimasomaso.

Usiku wa kuamkia Jumapili ya Oktoba, 30 jijini Mwanza kumefanyika mashindano ya Miss Tanzania 2016 ikiwa ni kwa mara ya kwanza tangu serikali ilipotangaza kuyafungua mashindano hayo Disemba, 2014.

Katika mashindano ya mwaka huu kama kawaida ya mashindano hayo walimbwende walipanda jukwaani na kuonyesha uwezo wao wa kutembelea kama ma’miss’ lakini pia uwezo wa kujibu maswali ambayo yaliandaliwa na majaji.

Baada ya mchakoto wote kukamilika, mwanadada ni Miss Kinondoni 2016, Diana Edward alitangazwa kuwa mshindi wa Miss Tanzania kwa mwaka 2016, nafasi ya pili ikishikiliwa na Maria Peter na mshindi wa tatu akiwa ni Grace Malikita.

Chapisha Maoni

0 Maoni