Nimejiridhisha, wanawake wanapenda mwanaume wa namna hii

1.Kwanza unapoanzisha mahusiano unatakiwa kujua mpenzi wako amewahi kuumizwa kwa kiasi gani huko nyuma, then unatakiwa uanze kumpa tumaini jipya kwa kuonesha wewe ni wa tofauti kwa vitendo


2.Anapokuwa yupo confused, unapofungua mdomo wako ongea madini ambayo yatamfanya aone njia ya kupita kutatua tatizo lake, hata Kama itabidi wewe utoe, usitoe tu kitu Kama unamfadhili ila tumia akili ajue unajali shida yake na umemsaidia kwa kuwa yeye mwenyew ameshindwa

3.Usimfanye aamini eti unajua kila kitu, au una pesa sana jitahidi umfanye ajue nini huwezi ila kuwa makini hapa usije akajua udhaifu wako uliomfanya aumie mwanzo

4.Kuwa mpole, mtaratibu na Muungwana, sometimes muone Kama binti yako, mpe ushauri muafaka huu ya maisha yake na mfanye aone mbele yenye
matumaini

5.Mjari, mpe anttetion, mseme anapokwenda kinyume (kwa maneno yasiyo ya mtaani, bali maneno yatakayomfanya ajisikie kuumia kwa alichokifanya, epuka kutoa machozi kipindi unaongea)

6.Acha utoto Wa kususa susa na kununa nuna anapokosea, kuwa muwazi kumwambia kipi hupendi kipi unapenda huku ukijitahidi kumfanya ajisikie wewe ni mtu wake wa karibu, mruhusu adeke

7.Epuka kuongea mambo ya kipuuzi puuzi,

8.Epuka kuvaa mikufu ,bangili,heleni na vingine vya kitoto kama mlegezo n.k, ila kuwa msafi, na vaa nguo safi zinazokutosha na kukupendeza

9Uwe karibu na nyumba za ibaada na sometimes unavyoongea naye ingizia mambo ya dini katika kumjenga zaidi

10.Mpe nafasi na msupport kwenye vitu anavyovipenda 'hobbies',
 

Chapisha Maoni

0 Maoni