SIMULIZI: Mtoto alivyookoa ndoa ya wazazi.

Maisha ya shost na mume wake hayakuwa mazuri kihivyo, wote walikuwa wajiiriwa wa serikali na walibahatika kupata watoto wawili, wakiume miaka mitano na wakike miaka mitatu. Kila wakikaa na mume wake walijaribu kujipanga jinsi ya kusomesha watoto, na kuwa hata na kibanda chao wenyewe badala ya kupanga nyumba.

Bi shost alifukuzia nafasi za masters kila zikitoka kazini, na alianza na maombi milango ifunguke. Wakisema kila kitu kina wakati wake si utani, siku shost alipopata waraka wa kumfahamisha anatakiwa kujiunga na chuo kikuu kilichopo Botswana kwa masomo yake ya shahada ya uzamili.

Walikaa chini na mume wake, wakapanga kuwa, akifanikiwa kumaliza masomo atafute kazi kule ili watoto wapate elimu bora pia waweze kuweka pesa ya kujenga nyumba nyumbani. Bishost alifanya tafrija kidogo ya kuwaaga ndugu na jamaa wa karibu na kuondoka.

Alikuwa na utaratibu wa kuongea na mume wake kila siku jioni na watoto weekend kwakuwa mara nyingi anapopata nafasi ya kupiga simu watoto wanakuwa wamelala. Miezi kama minne baada ya kuondoka tabia ya mume ikaanza kubadilika, anapopiga simu inakuwa imezimwa, akumuuliza ni visingizio vingi tu. Yule dada alitafakari hili akaamaua kumwambia mume wake, kama wewe uko busy, basi wanunulie watoto simu ili nikipiga niongee nao maana kama mama huwa sina amani nikiwa mbali nao.

Simu ilinunuliwa na baba akijua amepata nafuu ya kusumbuliwa. Sasa baba hakwenda mbali sana, Alianza kutoka na rafiki wa karibu sana wa bishost, anaeitwa Clara, aliyempa mkanda wote huo bishost ni mtoto wa kiume wa miaka mitano, kwa kifupi, Clara alianza kuplay mother figure kwa watoto, alimpeleka yule boy kwa dentist, weekend anawapeleka wakale ice cream, kwenye mabembea. Basi mtoto alianza kutiririka, mama akawa oh, mpe aunt Clara asante nyingi, akijua ni shost anamsaidia, zali lilikuja mtoto alipoendelea nitamwambia kesho akiamka, khe wewe kwani unalala kwake, hata si analala chumbani kwako.

Bi shost hakuongea na mtu, alinunua ticket na kuja na kumkuta kweli aunt Clara ameenea sitingroom akiangalia TV na mr akiwa na khanga moja. Ndoa ilisalimika na baba alikusanya watoto wote walielekea Botswana.
 

Chapisha Maoni

0 Maoni