Ahmed Salum: TRA hawakusanyi kodi, wanakusanya malimbikizo ya nyuma

Mbunge wa Solwa (CCM) Ahmed Salum, amedai Serikali imeweka sera mbovu kuhusiana na bandari kwa kuweka kodi ambazo zimewakimbiza wafanyabiashara pia amesema TRA hawakusanyi kodi ila wanakusanya malimbikizi ya nyuma na baada ya muda malimbikizi hayo yataisha na ukusanyaji utarudi bilioni 850 kama Kikwete alivyoacha.


Amesema washauri wa Magufuli hawamuambii ukweli kutokana na woga
Amesema sSngle Custom Territory na VAT kwenye transit goods zimewakimbiza wafanyabiashara na wafanyabiashara wamehamia bandari za nchi za jirani

Leo hii waziri wa fedha ameacha kodi za matrilioni bandarini wanaenda kukabana bodaboda na trafiki wanakusanya faini barabarani kama vita.

alisema hivi sasa kuna tatizo la mzunguko wa fedha katika jamii, huku akishangazwa na kauli ya Waziri Mpango ya uchumi kuimarika.
Alisema anashangazwa na taarifa ya kuimarika uchumi, japo bado kuna matatizo ya uchumi, ikiwamo upande wa wawekezaji wanaokuja nchini.
Mbunge huyo alisema hakuna kituo kimoja kwa ajili ya kuhakikisha wawekezaji hawasumbuliwi, lakini bado kuna tatizo Kituo cha Uwekezaji (TIC), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambao hukaa na nyaraka muda mrefu bila kufanya uamuzi.

Chapisha Maoni

0 Maoni