MADINI MAPYA YAGUNDULIWA MERERANI

Madini mapya yamegunduliwa hapa nchini, katika eneo la Mererani wilayani Simanjiro. Yamepewa jina Merelaniite.


Jina hilo limetokana na eneo ambalo madini hayo yamepatikana, Mererani katika milima ya Lelatema katika wilaya ya Simanjiro, Manyara.

Eneo hilo linafahamika sana kwa madini ya Tanzanite.

Madini hayo yaligunduliwa na wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Kiteknolojia cha Michigan cha Marekani.

Wataalamu sita waliofanya uchunguzi, kwenye makala iliyochapishwa kwenye jarida la Minerals (Madini) wanasema madini hayo yana vipande vinavyofanana na sharubu vya rangi ya kijivu vya urefu wa milimita moja hivi, ingawa kuna baadhi vyenye urefu wa hadi mililita 12.

Madini hayo yanakaribiana na madini ya zoisite (aina ya Tanzanite), prehnite, stilbite, chabazite, tremolite, diopside, quartz, calcite, graphite, alabandite na wurtzite.

Chapisha Maoni

0 Maoni