DC Kinondoni aagiza mwalimu mkuu avuliwe madaraka

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ali Salum Hapi,amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kumvua madaraka Mwalimu Mkuu wa Shule ya Mwananyamala B kwa kosa la kuruhusu kujengwa kwa mabanda ya biashara katika eneo la shule hiyo.



Mhe. Hapi ametoa agizo hilo katika ziara yake ya kutembelea maeneo mbalimbali katika kata ya Makumbusho ambapo amezitaka shule zote za wilaya hiyo kutokujenga mabanda ya biashara kwa kuwa mabanda hayo yanasababisha walimu kushindwa kufundishwa na kuanza kugombea mapato.

Aidha Mkuu huyo wa Wilaya amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa hiyo kuhakikisha ujenzi wa soko la Kisiwani uliokuwa umesimama kuhakikisha unaendelea ndani ya kipindi cha wiki mbili kuanzia jana.

Mhe. Hapi amesema kuwa ni jambo lisilokubalika serikali kutoa fedha kisha watu kuzikalia na kuacha kuzifanyia miradi ya maendeleo yanayohitajika ikiwemo ujenzi wa soko hilo.

Katika ziara yake hiyo Hapi ametembelea maeneo mbalimbali ikiwemo shule ya msingi Kisiwani, shule ya msingi Minanzini, shule ya Msingi Mwananyamala, soko la Kisiwani na soko la Mapinduzi.
 

Chapisha Maoni

0 Maoni