JPM AFUNGUKA, WIMBO WA MRISHO MPOTO-SIZONJE WAMKUNA.

Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefunguka yake ya moyoni kuwa, katika wasanii, anampenda sana Mrisho Mpoto na hasa wimbo wake wa SIZONJE ambao umeonekana kumkuna.

Akifunga mahojiano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa ikulu jijini Dar, Mhe. rais ameuomba wimbo huo mubashara na msanii Mrisho Mpoto, ambaye aliongeza vionjo ambavyo vimempa tabasamu lisilo nakifani.

Chapisha Maoni

0 Maoni