Bakwata wasema JPM anawabagua waislam, Sheikh Khalifa Khamis aishtumu TRA

Sheikh maarufu nchini Khalifa Khamis ameishtumu Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) kuwa ina lengo la kuikwamisha dini ya Kiislam. Ameishtumu TRA kuwa na masharti ya kibaguzi dhidi ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania, amesema masharti hayo yamejaa hila, udhalilishaji. Amedai nia ya TRA ni kukwamisha shughuli za BAKWATA hapa nchini kwa kisingizio cha kodi za magari lakini nia yao kukwamisha dini ya Kiislamu.


Amezitaka taasisi za Kiislamu nchini kukataa maagizo kutoka TRA.

Pia ameishtumu Serikali ya awamu ya 5 kuwa inawanyima waumini wa dini ya kiislamu nyadhifa katika teuzi mbalimbali na amesema kuwa baadhi ya Waislamu wamekuwa wakiondolewa nafasi zao serikalini sababu ya dini yao.

Ameongeza kwa kuitaka Serikali ibadilishe sheria ya ugaidi nchini kwa sababu ni kandamizi na Waislamu wengi wamekuwa wakikamatwa kwa kisingizio cha kuwa magaidi na hawapelekwi mahakamani na mpaka sasa kuna baadhi wako jela bila kufikishwa mahakamani, ametoa mfano wa masheikh wa Zanzibar wanaoshikiliwa kwa muda mrefu bila kufikishwa mahakamani.


Chapisha Maoni

0 Maoni