CCM kumuweka meya wa CHADEMA Kigamboni

CHAMA cha Demokrasia na maendeleo (Chadema), kipo katika mkakati mzito wa kuhakikisha Kamati kuu ya Chama cha Mapinduzi(CCM),inayoanza kikao chake leo jijini Dar esSalaam, kinampitisha Dotto Msawa,ambaye ni diwani wa Kigamboni CCM,kuwa mgombea wa nafasi ya Umeya wa Manispaa mpya ya Kigamboni kwa ajili ya kuweka mazingira mazuri ya kuwa na turufu katika maamuzi mbali mbali ya jiji la Dar sSalaam kwa mambo yatakayohitaji uamuzi wa kupiga kura


Taaria za uhakika toka ndani ya Chama hicho zinadokeza kuwa,tayari mkakati huo unasimamiwa na watu wa Karibu wa waziri mkuu aliyejiuzulu Edward Lowasa kwa kuzingatia ukaribu wao wakati Lowasa alipokuwa CCM

Inaelezwa kuwa moja ya mikakati ya kuhakikisha kamati kuu inampitisha Msawa, ni pamoja na diwani huyo kushambuliwa kwa maneno na kuibuliwa kwa kashfa zake mbali mbali kupitia gazeti la Tanzania Daima linalomilikiwa na mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe.

“Chadema kwa Manispaa ya Kigamboni haina chake kwani madiwani wa Ukawa ni wachache hivyo mkakati wao umelenga katika dhana nzima ya Rais Magufuli kuwapitishia mtu wao kupitia kauli yake kuwa ukiona wapinzani wako wanamshambulia sana mtu wako basi huyo ndiyo umpe nafasi na sasa hivi kama unafuatilia utajua namna mkakakti huo ulivyofanikishwa kwa kina na gazeti la Tanzania Daima”kilidokeza chanzo cha habari hizi .

Msawa anayetajwa kuwa swahiba wa Karibu wa Edward Lowasa, katika mkakati huo anatajwa kuwatishia gazeti la Tanzania Daima kuwa atawapeleka mahakamani kwa kumchafua lengo lilikwa ni kukuza mjadala wa jina lake kabla ya kamati kuu ya CCM haijafanya uteuzi wa jina la mgombea umeya wa Kigamboni

Kwa zaidi ya wiki tatu sasa gazeti la Tanzania Daima limekuwa likiaandika taarifa zinazomhusu Dotto Msawa ikiwa ni pamoja na kuweka vielelezo vya namna alivyofikishwa mahakamani mkoani Morogoro Mwaka 2011 akihusishwa katika wizi wa gari      

Chapisha Maoni

0 Maoni