Kupatwa kwa Baba Levo: Shilole Kiuno ampa vijembe Baba Levo, asema kwake ni kama mwanamke mwenzake

Msanii Shilole Kiuno ambaye  ametimiza miaka 28 amefunguka na kusema kuwa msanii Baba Levo ni kama mwanamke mwenzake >wakati akifanyiwa mahojiano na Planet Bongo ya EA Radio. Shishi alidai kwani hata akilala naye mpaka asubuhi kitanda kimoja Baba Levo hawezi kumfanya lolote kutokana na jinsi wanavyo heshimiana.
15624451_385159655159071_3397786530951987200_n
Shilole
Mbali na povu hilo, kwa siku ya jana ambayo ni Disemba 19, Msanii Baba Levo ambaye ni mtu wa karibu wa msanii Shilole, alisema msanii huyo katika siku za hivi karibuni amekuwa akifanya mambo yanayomkera.
Baba Levo aliyasema hayo alipofanya mahojiano na kipindi cha eNewz ya kituo hicho hicho na kusema kuwa mambo anayoyafanya Shilole yanamlazimu akae mbali naye, ili kujiepusha na lawama.
“Shilole kuna baadhi ya vitu ananiudhi, sasa hivi ana nguvu kubwa na umaarufu mkubwa kwenye mikoa wa kufanya show na kuingiza hela nyingi, kwa hiyo mimi nilikuwa nataka tutumie hiyo timing kutengeneza pesa, kama marafiki ye akitengeneza pesa na mimi nitapata pia, lakini unaona anajifanyia vitu kama uhanangwa uhanangwa, mara kafanya hivi mara hivi, sasa ili usigombane naye unakaa mbali naye, kama unamshauri mtu kitu hafuati huo ni uhanangwa”, alisema Baba Levo.
Baba Levo aliendelea kusema kuwa tabia ya msanii huyo ya kubadilisha wanaume kila siku kwake haina tatizo kwani Shilole ni msichana mrembo hivyo ana kila sababu ya kupendwa na kuchagua maisha yake.
“Shilole ni msichana mzuri, ukitoka wewe ukajifanya humtaki anakuja mwingine anampenda sana, ni maisha amejichagulia anataka kuishi kama Lady Gaga, hata kama alikuwa anafanya mambo ya kihanangwa ni kuweka mambo yake hadharani”, alisema Baba Levo,  anapoweka mambo yake mitandaoni si kitu kizuri”.

Chapisha Maoni

0 Maoni