Dar es Salaam. Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo,
maarufu Mzee wa Upako amesema waandishi wote wanaoandika habari za
kumchafua watakufa kabla ya kufika Machi mwakani.
Kauli hiyo aliitoa jana ikiwa ni mwendelezo wa mahubiri yake ya nne
katika wiki ya tatu mfululizo, akijibu yaliyoandikwa kwenye vyombo vya
habari kuhusu kumfanyia fujo jirani yake na kulewa.
“Kila mwandishi aliyeniandika vibaya ikifika mwezi wa tatu akiwa hai,
mimi naacha kuhubiri, nafunga virago nakwenda kuuza gongo, sasa Mungu
ndiye ataamua kwamba ama niache kuhubiri mimi au wewe ufe …najua hata
leo mpo humu mmekuja na mnasikiliza tu,” alisema.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA