Phil Jones asema yake ya moyoni kuhusu Fellaini

Wachezaji wa klabu ya Manchester United, wamekasirishwa sana kwa kitendo cha Marouane Fellaini kuzomewa uwanjani. Fellaine ni kiungo wa timu hiyo anayelaumiwa kwa kusababisha penati iliyosaidia klabu ya soka ya Everton kusawazisha goli walipomenyana hivi karibuni.


Wapenzi na mashabiki wa United walionekana kuchukizwa na kitendo kile na walimzomea wakati alipoingizwa kwenye kipindi cha pili cha mechi dhidi ya Tottenham mwishoni mwa juma kadhaa.

Phil Jones alisema kwamba wachezaji hawakufurahishwa na kitendo cha Fellaini kuzomewa na mashabiki.

Wachezaji wenzake wanaamini kwamba Fellaini hakutendewa haki na mashabiki wao.

Chapisha Maoni

0 Maoni