Serikali
imesema haitambui mkataba wowote wa ajira uliotolewa baada ya Mei Mosi,
kwa kuwa suala hilo lilizuiwa kuanzia siku hiyo ili kupisha uhakiki wa
watumishi hewa.
Msimamo huo ulitolewa jana na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma, Dk Laurean Ndumbaro alipotoa ufafanuzi kuhusu
wataalamu wa mifugo walioajiriwa Mei 2, na taarifa zilizozagaa kwenye
mitandao ya kijamii kwamba amefuta ajira za walioajiriwa Juni.
“Ajira zote zilisitishwa Mei Mosi kupisha msako wa watumishi hewa.
Yeyote aliyepewa barua ya ajira baada ya hapo ni kama hakupewa kitu,”
alisema Dk Ndumbaro.
CHANZO: Mwananchi
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA