Hizi ndege hata marubani wanaziogopa!!!Maana zipo "kisiasa" sana.Kila
mtu anatafuta pa kupatia "kick" linapokuja suala la ATCL.Kilichotokea
Kisongo ni jambo la kawaida sana ktk usafiri wa anga.
Hapo ni suala la kawaida sana,wakati wa kutua rubani alikuwa anataka
kupiga turning ili aingie Apron(sehemu ya maegesho ya ndege)kwa ajili ya
kushusha abiria,lkn bahati mbaya tairi moja la nyuma likatoka nje ya
runway.
Sasa kwa sbb hizi ni ndege mpya;jamaa akaona isiwe tabu,ni bora asubiri
"Towing Car" ili aweze kuitoa.Angeweza kuitoa hata kwa ku-tax,lkn
amechukua tahadhari ili kuepuka lawama.
Na kwa sbb uwanja wa Kisongo ni 12hrs,hufunguliwa na kufungwa wakati wa
mawio(sunrise) na wakati wa machweo(sunset),kwa muda iliofika Kisongo na
kutaka kuondoka ndege isingeweza sbb muda wa kufungwa uwanja
ulishafika,na Kisonge haina taa za sehemu ya kutua na kurukia,kama
ingalikuwapo "dear bombadia" ingerudi Dsm usiku kwa usiku.
Hali hii ipo Mtwara,Kigoma,Tabora na hata Mbeya.Ndio maana kuna safari
ikitokea itilafu kidogo tu na ikafika saa kumi jioni Fastjet bado ipo
Dsm haiwezi kwenda tena Mbeya.
Safety First,hiki ndicho rubani kazingatia,angeweza kulazimisha kukata
kona na kuitoa,lkn alitaka kuhakikisha kuwa abiria wote wanashuka kwanza
ili kupunguza uzito.Yangetokea mengine ndio watu wangelaumu sana.
Incidence za kubasti tairi,kuchepuka nje ya runway au taxway ni za
kawaida sana,ni kwa sbb huwa haziripotiwi au ni kwa vile zimetokea kwa
ATCL ndio maana zinashika kasi na heading mitandaoni.
Rubani kafanya maamuzi sahihi...
Na hii ni incidence ya kawaida sana ktk usafiri wa anga.Hapa juzi kati
huko Nairobi ndege ilipata tatizo kwenye Runway na uwanja ukafungwa
zaidi ya masaa 6,ndege zote za Jomo Kenyata zikawa diverted KIA na Dsm
hadi uwanja ulipofunguliwa.
Siku kadhaa zilizopita zililetwa habari za Oman Air kupata mpasuko wa
tairi huko Dsm.Waarabu wa Oman walikaa kimya huku wakiendelea na
uchunguzi,hawakupiga mayowe ili wasipoteze abiria wa ndege zao ambao
wamekuwa wakizitumia kufika Asia na mashariki ya mbali.Kusafrisha
mahujaji nk.Walikaa kimya sbb,basti ni kitu ya kawaida,na kwao ndege ni
sehemu ya utalii na kipato cha nchi.Sasa sisi kuchepuka tu kwenye
taxway/runway ni maneno ya kejeli tupu.
Masaa sita ni mengi;kwanza yanaonyesha pengine nchi husika haijajiandaa
kukabiliana na dharula,majanga ya moto na ajali.Lakini vyombo vya Kenya
wala havikushobokea habari hii,ilipita kimyakimya sbb wanajua madhara
yake.Hii si "habari" kwa maana ya ndani ya Taifa la kwao.Linawashushia
heshima ya utayari ktk majanga na uokozi.Wakaipiga "pini" na kujadili
mambo mengine.
Sisi Bombadia rubani kafanya tahadhari ya kuepusha majanga kwenye
"landing gears" basi kila mahali usiku huu n maneno na "kuiponda"
ATCL!!Ebooooo!!Tabia gani hii ya kutokilinda vya kwenu?Ndege haina "side
mirror",ilimpasa kujiridhisha ili kuiweka ndege ktk sehemu
salama.Lakini watu wameanza kusema na mengine ambayo hata hayapo.
Hii ni kitu ya kawaida,ndio maana kuna incidence na accident!!Ila kwa
sbb ni ATCL,watu wataongea sana saanaaa.Lkn hao hao wapiga kelele ndio
wa kwanza kukuomba uwafanyie booking ya ATCL.Loooh!!Pole sana
ATCL...Unaonekana "yatima" hata ktk ardhi ya mama yako Tanzania.Huu sasa
sio ukosoaji,ni MASIMANGO!!Kutwa kucha kuisimanga ATCL...Duuuh!!
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA