TAFAKURI: Mawaziri Charles Mwijage na Sospeter Muhongo wamepotosha, umma Dangote hajawahi kutaka gesi ya Bure

Mawaziri wa Sopeter Mhongo na Charls Mwijage wamepotosha Umma wiki nzima wakidai kuwa Kampuni ya cement ya Dangote ilikuwa inataka ipewe gesi ya bure toka Mtwara ambako hicho kiwanda kilipo na ambako pia gesi inakotoka kuja Dar es Salaam.


Mawaziri hawa amekuwa akitumia lugha za vitisho na ubabe kuelezea hili sakata lakini kuna ukweli ambao wamekuwa wakiuficha na hawajataka kuelezea.

1. Dangote kulazimishwa kutumia makaa ya mawe ya Kiwira na Liganga:


Hakuna mahala kwenye mkataba wa Dangote na serikali ya Tanzania ambako Kampuni ya Dangote wanalazimishwa kutumia malighafi za ndani ya nchi. Sasa kwa nini Dangote alazimishwe kutumia makaa ya mate ya kiwira? Kwa nini waziri Mwijage hatajataja sheria inatolazimisha mwekezaji kutu mwekezaji kutumia malighafi za ndani ya Tanzania?

Binafsi sioni tatizo lolote la Dangote kuagiza hayo makaa ya mawe. Akiagiza toka China au Ukraine au India au Russia au hata mwezini mimi sioni tatizi ili mradi ametimiza masharti ya ya uwekezaji, anazalisha bidhaa inayoweza kununulika na wananchi maskini wa kipato waliopo ndani ya Tanzania, analipa kodi, ameajiri Watanzania, waajirwa wake wanalipa kodi, anafanya Corporate social responsibility (CSR), kampuni yake inafanya technology transfer, anachangia kwenye maendeleo ya taifa hili.

Mshajiuliza mbona kampuni za Bakhressa zinanunua ngano toka Canada na Australia? Mbona viwanda vya pombe nchi kama TBL hii wanaagiza malighafi zao toka Africa ya kusini wakati Arusha mashamba ya hiyo malighafi yapo? IPP pia nao huagiza malighafi zao nje ya nchi na viwanda vinginevyo pia sasa kwa nini hawa mawaziri hajalalamika? waziri aliyelalamika?

2. Why Kiwira na Liganga?

Hivi mshajiuliza kwa nini hakuna ayenunua hayo makaa ya mate ya Liganga au Kiwira? If I remember correctly tuliambiwa kuwa nao ni investors in the same calibre kama Dangote sasa why hawa export hayo makaa nje ya nchi badala ya ku lobby na kulia lia kwa mawaziri ili Dangote anunue makaa yao ya mawe?

3. Dangote anataka makaa ya mawe ya bure


Hawa mawaziri kwa nyakati mbali mbali wiki hii wamekuwa wakitoa tuhuma kuwa Dangote walitaka gesi ya BURE toka Mtwara. Hii nayo si kweli kwa sababu moja ya hizo incentives alizopewa kama strategic investor ni reasonably priced gas (unafuu wa bei) kwa sababu ya proximity (ukaribu) ya kiwanda cha Dangote na chanzo cha gesi (hii ilikuwa ni moja ya sababu kubwa Kiwanda kujengwa Mtwara) .

Kilichotokea ni TPDC walitaka kuizia Dangote gesi kwa bei ya viwanda ambavyo viko kilomita 542 Dar kama Wazo n.k. Hili kuala la TPDC lilingiliwa na Titus Kaguo wa EWURA kwenye vikao mbali mbali vilivyofanyika huko Mtwara na Mkuu wa Mkoa na moja ya maazimio ya kikao chao cha mrisho walichokaa kati ya Dangote, Wizara ya nishati, wizara ya biashara,TPDC, TIC, EURA, serikali ya Wilaya, na Mkoani ni kuwa TPDC wafanye upembenuzi yakinifu juu ya bei kisha wapeleke repoti yao (ambayo mpaka sasa hivi ninavyoandika huu uzi haikupelekwa)

4. Bei ya gesi
As it is sasa hivi bei ya hiyo gesi ya TPDC ni $ 2.14 per 1000 cubic feet. na bei hii inajumisha processing,transportation na distribution hivyo akina Kaguo wao walitaka bei wanayotoza iwe uniform nchi nzima. Mfano una kiwanda chako karibu na chanzo cha gesi utalipa bei sawa na mtu ambaye kiwanda chake kiko Horohoro Tanga au Kigoma.

Pia kwa kuongezea tuu ni kuwa sasa hivi baada ya malalamiko toka kwa watu wa Mtwara TPDC wameweka categories 6 ya kilomita 100 toka huko inakozalishwa gesi (Mtwara) na kwenye categori ya kwanza inamhusu ni watu walio karibu na chanzo cha gesi na Dangote anaingia kwenye categori hiyo na bei zao zitakuwa significantly lower (chini) tofauti na wengine. Lakini niongozee tuu kuwa kwa kuwa serikali sasa hivi ina matatizo ya pesa hivyo wameamua kuweka tariff nyingine ya $3 juu ya ile mwanzo ambayo ni $ 2.14. Naomba niweke wazi kuwa hiyo $3 haikuidhinishwa na EWURA na haijulikani kuwa hili $3 inaenda kwa nani na inafanya nini na justification yake ni nini

Hivyo hakuna ukweli kuwa Dangote alitaka gesi ya bure!

5. Dangote na Umeme wa TANESCO

Kuna watu watauliza kwa nini Dangote asitumie umeme wa TANESCO? ukweli ni kuwa hao Tanesco walikaa chini na Dangote lakini kwa kuwa hawakuwa serious kwa sababu supply line yao ya Mtwara kva33 wakati kiwanda cha dangle kina mahitaji ya kva 132 hivyo option ya Tanesco ikafa. Na Tanesco hawajaona umuhimu wa kuongeza capacity kule capo wangeweka walau kwa umeme wa kva 200 wangeuza kwa Dangote na mwingine kwa viwanda vingine na mwingine wange sambaza kwa raia.

6. Kwa nini Dangote hawajalalamika?


Hawa Dangote wamekuwa wakiteseka sana tena kimya kimya kwa sababu political leadership yetu hawako serious na wanataka kila kitu wafanyiwe na Mheshimiwa Magufuli. Na hawa watu tunaambiwa wana PhD's za kila namna.

Dangote ni serious investor na sioni kwa nini hawa mawaziri wamekuwa hot headed kudeal na kampuni hii wakati tunasema tunataka kuwa na uchumi wa viwanda na huku tuna ndoto za kuwa na viwanda vikubwa vya wawekezaji wa ndani na wanje kama akina MAINDRA, GE, FORD, VW, TATA, AIRBUS na wengineo .

WAY FORWARD:
1. Serikali ivunje TIC na badala yake kila mkoa uwe na Investment Centre yake ambayo itakuwa ina coordinate na wizara ya viwanda directly na kila mkoa uwe na mikakati ya kujiendeleza badala ya kutegemea hawa miungu watu waliojazana Dar es salaam ambao hawana interest kabisa na hawa wawekezaji au huko investments zinakopelekwa

2. Serikali ivunje au reform BRELA completely from scratch. Haiwezekani mtu ukitaka kufanya simple search kutaka kujua directors au who is who Dangote Tanzania unaambiwa kwenye website ya BRELA ujiandikishe,awake namba yako ya simu, tarehe yako ya kuzaliwa, unakoishi etc ili kufanya simple search ya kampuni. Hu ni urasimu usio na maana. Search should mean search kama vile unaingia google unasearch jamiiforums na unapata results bila kuambiwa ku register na kutoa private info zake

3. Wizara ya Viwanda lazima ifumuliwe completely. Serikali ipunguze wafanyakazi (yes this is unpopular opinion na wale ambao wanaona ni birthright yao kufanya kazi serikalini) badala yake serikali i invest kwenye technology na kuondoa urasimu.

4. Serikali set up Foreign Investment Review Authority ambayo itakuwa inashauri serikali kwenye mambo ya Foreign Investment Policy (the Policy). Hiki combo kingekuwepo sidhani kama haya mazingaombwe ya akina Muhongo na Mwigaje yangetokea

5. Kama tunataka sana hawa wawekezaji wtumie malighafi zetu then why not have LOCAL CONTENT ACT? Kwa nini serikali haitaki kuleta hiyo Act ili tujue kuwa kwenye kila kitu priority iwe mTanzania na Rasilimali/malighafi za Tanzania?

6. Tuache siasa kwenye uchumi.      



Chapisha Maoni

0 Maoni