Aua kichanga na kukifukia shimoni


Na Omary Mngindo, Chalinze
MKAZI wa Kitongoji Magwila Kata ya Bwilingu Halmashauri ya Chalinze, Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani Fatuma Ramadhani (32), anashikiliwa na jeshi la Polisi kwa tuhuma za kujifungua kitoto jinsia ya kike cha miezi 6 kisha kukifukia kwenye shimo.



Mtuhumiwa Fatuma Ramadhani

Wakizungumza na mwandishi wa habari eneo la tukio, mashuhuda Mwanamosi Mohamed mjumbe wa nyumba kumi alisema kuwa alipata taarifa ya tukio asubuhi saa 3 ya Mei 27 akijulishwa kuwepo kwa mama anayetuhumiwa kujifungua kitoto hicho kisha kukifukia kwenye shimo alilochimba jirani na choo cha nyumba anayoishi.

"Nimepigiwa si unammoja wa wakazi akinijuza kuhusiana na tukio hili la mwanamke kujifungua kisha kuchimba shimo dodo kukifukia, nikiwa mjumbe wa nyumba kumi nimejulishwa kutokea kwa tatizo hili, nikampigi Mwenyekiti wa Kitongoji naye akatoa taarifa Polisi na kwa Mganga Mkuu wa Kituo cha afya cha Bwilingu," alisema Mwanamosi.


Mganga Mkuu wa Kituo cha afya Dkt. Waziri Waziri alisema kuwa uchunguzi wake amebaini kuwa mtuhumiwa huyo amedhamilia kufanya tukio hilo huku akibainisha kwamba kitendo chake cha kuweza kuchimba shimo dogo kisha kufukia inaonesha alikusudia jambo hilo.

"Nitoe wito kwa wanawake kujiunga na uzazi wa Mpango, hatua hii itasaidia kuwawezesha kujipangia uzazi watakavyo ukilinganisha na matukio kama haya yanayosababisha mlengwa kufanya tukio la kuua kitoto," alisema Dkt. Waziri.

Mwenyekiti wa Kitongoji Said Halfan alisema kwamba alijulishwa kutokea kwa tukio hilo, alifika enro la tukio kushuhudia hali hiyo kisha akatoa taarifa kwa Mkuu wa Kituo cha Polisi na Mganga Mkuu wa Kituo cha Bwilingu ili kuanza kufuatilia taratibu za kitaalamu.

"Kama unavyoshuhudia askari na mfanga wapo hapa kwa taratibu za kitaalam, baada ya taratibu tumeambiwa tukihifadhi hapahaoa hiki kiumbe, tukio limenidikitisha saha, nitumie fursa hii kuwaomba wanawake kuacha tabia ya kutoa mimva au kuuwa viumbe kama mkazi huyu," alisema Halfani.


Akizungumza na mwandishiwa habari, Fatuma alusema kwamba ilipofika saa 11 alfajili alianza kujisikia msumivu makali kabla ya kujifungua kwa bahati mbaya na kwamba huo ni uzazi wake wa tatu.

"Hii hali hata mimi imenishtua kwa sikutarajia kukutwa na tukio kama hili, ghafla nikiwa ndani ya chumba nikajisikia maumivu makali wakati nataka kuita wapangaji wenzangu ghafla nikajikuta nimejifungua," alisrma Fatuma.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Obesmo Lyanga amethibitidha kuwepo kwa tukio hilo na kwamba uchunguxi zaidi wa tukio hilo unaendelea kabla ya kufikishwa mahakamani.

Chapisha Maoni

0 Maoni