Taifa Stars yajifua kisawasawa Jijini Alexandria, Misri

 Libero wa Taifa Stars, Erasto Nyoni (katikati) akijitahidi kudhibiti mpira mbele ya washambuliaji wenye njaa ya kufunga, Ibrahim Ajib (kulia) na Abderheman Mussa kabla ya kipa Said Mohammed hajatokea kusaidia wakati wa mazoezi ya timu hiyo yanayofanyika Kituo cha michezo cha Tolip (Tolip Sports City) hapa Alexandria, Misri.



  Kiungo wa pembeni wa Taifa Stars, Simon Msuva akiwa kwenye kasi kuwahi mpira wakati wa mazoezi ya timu hiyo yanayofanyika Kituo cha michezo cha Tolip (Tolip Sports City) hapa Alexandria, Misri.

  Kipa Said Mohammed Nduda , akichupa kuzuia mpira wakati wa mazoezi yanayosimamiwa na Kocha wa Makipa wa Taifa Stars, Patrick Mwangata aliyepiga magoti katika mazoezi yanayofanyika Kituo cha michezo cha Tolip (Tolip Sports City) hapa Alexandria, Misri.

 Kipa Aishi Manula, akichupa kudaka mpira wakati wa mazoezi yanayosimamiwa na Kocha wa Makipa wa Taifa Stars, Patrick Mwangata aliyepiga magoti katika mazoezi yanayofanyika Kituo cha michezo cha Tolip (Tolip Sports City) hapa Alexandria, Misri. Taifa Stars  inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti inayozalishwa na Kampuni ya Bia ya SBL, inajiandaa kucheza na Lesotho Juni 10, 2017 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataiafa ya Afrika (AFCON) za mwaka 2019 zitakazofanyika Cameroon.

Chapisha Maoni

0 Maoni