Wastara: Napitia Katika Wakati Mgumu kwa Sababu ya Sajuki


Msanii wa filamu za bongo Wastara Juma ambaye alikuwa mke wa marehemu Sajuki, ambaye alikuwa mke wa muigizaji marehemu Sajuki, amesema sasa hivi anapitia katika wakati mgumu sana kwa sababu ya Sajuki.
Akizungumza kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa na ukurasa wa facebook wa East Africa Television, na kusema kwamba Sajuki alikuwa kila kitu kwake, na hivi sasa kwa kuwa hayupo tena, ndio sababu anapata wakati mgumu na kumwaga chozi kila akimkumbuka.

Wastara aliendelea kwa kusema kwamba Sajuki alikuwa akimtetea na kumuangalia kwa macho yote, na kuwajibika kwa kuhakikisha kwamba hakuna jambo ambalo litamkuta mke wake na kumfanya aumie, lakini kwa sasa hana wa kumtetea.

“Sajuki ananipa wakati mgumu sana kwenye maisha yangu, alikuwa na nafasi kubwa kwangu, kwenye utendaji wa kazi, pili alikuwa ana jukumu kubwa la kumuangalia Wastara, nilikuwa kama mtoto wake, mimi nilikuwa fighter sana kwenye familia yangu, hivyo alihakikkisha siumizwi na lolote, hayupo tena mtu wa namna hii sasa hivi kwenye maisha yangu, naweza nikatetea wenzangu lakini nikiumizwa mimi sina wa kunitetea, lakini yeye alikuwa anacover nafasi zote, anahakikisha mke wangu haumizwi na kitu chochote”, amesema Wastara.

Wawili hawa walifunga ndoa ambayo iliwashangaza wengi baada ya kupata ajali na Wastara kukatwa mguu, lakini Sajuki alikubali kumuoa akiwa kwenye kiti cha matairi, bila kujali ulemavu alioupata, na watu kuamini kuwa Sajuki alikuwa na mapenzi ya kipekee kwa Wastara, kwa kutomuacha kwenye kipindi kigumu alichokuwa akipitia.

Chapisha Maoni

0 Maoni