Gavana BOT atangaza Serikali kuichukua na kuisimamia Benki ya Twiga Bancorp

Leo Oktoba 28, 2016 Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Profesa Benno Ndulu jioni hii anaongea na wana habari kwa suala lililoelezwa na BoT kuwa ni la dharura.

Taarifa rasmi kuhusu Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kuchukua usimamizi wa Benki ya Twiga hii hapa:
=======
Prof. Ndulu: Tumeamua kuchukua usimamizi wa Bank ya Twiga Bancorp kuanzia leo kutokana na upungufu wa mtaji wa benki hiyo.

Prof. Ndulu: BOT imekuchukua usimamizi wa benki ya Twiga baada ya kubaini upungufu mkubwa wa mtaji kinyume na matakwa ya sheria ya mabenki.

Prof. Ndulu: Shughuli zote za kibenki za banki hiyo zitasimamiwa na msimamizi kutoka Benki Kuu ya Tanzania.

Prof. Ndulu: Tutaisimamia benki hiyo mpaka atakapopatikana muwekezaji wa kuendesha shughuli zote za kibenki hiyo.

Prof. Ndulu: BOT itaendelea kutoa huduma kwa benki ya Twiga kutahatarisha usalama wa amana za wateja wake.

Prof. Ndulu: BoT itaendelea kulinda maslahi ya wenye amana ktk mabenki kwa lengo la kuleta ustahimilivu ktk sekta ya fedha 

Chapisha Maoni

0 Maoni