Baraza la Mitihani Tanzania jana tarehe 27 lilitangaza matokeo ya mitihani ya
darasa la saba kwa mwaka 2016 huku ufaulu ukiwa umeongezeka kwa asilimia
2.52 ukilinganisha na ufaulu wa mwaka jana huku shule ya msingi Kwema
iliyoko Mkoani Shinyanga ikiongoza Kitaifa.
KUANGALIA MATOKEO, BOFYA HAPA
Akitangaza matokeo hayo Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania
Dr Charles Msonde amesema kuwa jumla ya watahiniwa 555,291 kati ya
7789,479 waliofanya mtihani huo wamefaulu huku huku idadi hiyo ikiwa ni
sawa na asilimia 70.36 ambapo kati yao wasichana wakiwa ni 283,751 huku
idadi ya wavulana ikiwa ni 271,540.
Dk. Msonde pia alizungumzia baadhi ya shule zilizobainika kufanya udanganyifu na kufutiwa matokeo yao.
Shule kumi bora zilizofanya vizuri kitaifa katika matokeo hayo ni Kwema
na Rocken Hill za Shinyanga Mugini ya Mwanza, Fountain of Joy na
Tusiime za Dar es salaam na Mudio Islamic ya Kilimanjaro. Nyingine ni
Atlas ya Dar es salaam, St Achileus ya Kagera, Gft Skillfull ya Dar es
salaam na Carmel ya Morogoro.
Aidha Shule kumi zilizofanya vibaya katika matokeo hayo ni Mgata ya
Morogoro, Kitengu Morogoro, Lumba chini Morogoro, Zege ya Tanga na
Kilole pia ya Tanga. Nyingine ni Magunga ya Morogoro, Nchinila ya
Manyara, Mwabalebi ya Simiyu, Ilorienito ya Arusha na Chochero ya
Morogoro.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA