Habari zilizotufikia hivi punde ni kwamba watu zaidi ya 10 wamepoteza
maisha katika ajali iliyohusisha gari aina ya Noah iliyokuwa inatoka
Nzega kuelekea Tinde na Lori aina ya Scania lililokuwa linatoka Kahama
kuelekea Dar es salaam.
Ajali hiyo imetokea majira ya mbili kasorobo usiku leo Jumapili,November
06,2016 katika eneo la Nsalala kata ya Tinde mkoani Shinyanga.
"Waliopoteza maisha ni wengi sana,wapo zaidi ya 10,ajali inatisha",kimesema chanzo chetu cha habari .
Majeruhi wanakimbizwa hospitali ya mkoa wa Shinyanga.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA