Leo kwenye kipindi cha maswali na majibu, Mbunge wa jimbo la Hai na mwenyekiti wa kambi rasmi ya upinzani amepata fursa ya kuuliza swali kwa Mhe. waziri mkuu, ambapo swali lake lilimtaka waziri mkuu athibitishe juu ya kile kinachodaiwa kufanyika mkutano usiku wa wabunge wote wa CCM ukiongozwa na waziri mkuu mwenyewe pamoja na katibu mkuu chama cha mapinduzi Comrade Abdurahman Kinana.
Kikao hicho, pamoja na mambo mengine, kilijadili yale yanayoendelea bungeni pamoja na kutoa zawadi ya milion kumi kwa wabunge wa CCM ambao ni viongozi wa umma na wanabanwa na sheria ya utumishi wa umma namba 13 ya mwaka 1993. Swali la mhe. Mbowe lilimtaka waziri mkuu ajibu, je ni kweli tuhuma hizo na kikao hicho kilifanyika?
Naibu spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr. Akson Tulia, kama kawaida yake, ameinuka na kumkingia kifua waziri mkuu kutokulijibu swali hilo kwa madai kuwa, swali hilo liko nje ya sera, na maswali ya sera pekee ndiyo yatakayopewa fursa ya kupatiwa majibu.
Kwa mara nyingine, Mhe. Mbowe alisimama na kufafanua kuwa, ubadhilifu ama ufisadi ni masuala yalimo ndani ya sera hivyo msimamo wake ulikuwa ni kumtaka waziri mkuu ajibu swali hilo kama maswali mengine.
Msimamo wa naibu spika wa Bunge Dr Tulia ulikuwa ni kulikataa swali hilo na kuruhusu maswali mengine yaulizwe yaliyomo ndani ya sera, kama alivyodai, na hivyo swali hilo lilibaki bila majibu na kutaka kuleta tafrani ndani ya bunge leo hii. SIKILIZA MALUMBANO HAYO HAPA CHINI
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA