MAYALA: Mhe. Rais, ulipata wapi mamlaka ya kuzuia mikutano ya kisiasa wakati katiba haikupi nafasi ya kufanya hivyo?

Swali kutoka kwa Mr. Mayala, mtangazaji wa kujitegemea, kipindi cha mahojiano ya moja kwa moja leo kwenye ukumbi wa ikulu kati ya waandishi wa habari limeonekana kuumiza akili ya Mhe. rais, na hapo imembidi atumie kanuni ile isemayo, 'if they don't understand you, confuse them' ambayo kifalsafa imekuwa ikitumiwa mara nyingi na watu mashuhuri.
Swali liliuliza hivi:
Mh. Rais uliapa kulinda katiba ya Jamhuri ya Muungano wa TZ, Je ulipata wapi mamlaka ya kuzuia mikutano ya siasa wakat katiba haikupi nafasi ya kufanya hivyo?
Jibu....

'Mayala kwa kisukuma ni njaa, na wewe yawezekana ulizaliwa kipindi cha njaa' Wote wakacheka, akaendelea....
Mh. Mayala uliwahi kujiuliza kwa nini hotuba yangu ya kwanza ya kubana matumizi niliitolea Bungeni Mbele ya Spika? Ukijua mpikaji wa chakula ni nani na mgawaji wa chakula ni nani basi utanielewa.


Hili jibu, kwa mujibu wa wachambuzi wengi wa masuala ya kisiasa kwenye majamvi mbalimbali limetafsiriwa kama ni kutaka kuhakikisha jibu liwe gumu kwenye swali linaloelekea kwenye ukweli.

Chapisha Maoni

0 Maoni