Taarifa za kiintelijensia, hapa mjini Dodoma, zinaonesha kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe, amempa 'kazi maalum' Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA na Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni Tundu Lissu ya kushughulikia kashfa ya Wabunge wa CCM kuhongwa shilingi milioni 10. MAHENGA BLOG imedokezwa...
Jana, Mbowe aliwatuhumu Wabunge wa CCM kuhongwa shilingi milioni 10 kila mmoja ili waweze kupitisha Muswada wenye ubishani mkali wa Sheria ya Vyombo vya Habari. Mbowe, pamoja na kuzuiwa na Naibu Spika Dr. Tulia kuuuliza swali lake kwa Waziri Mkuu kuhusu kashfa hiyo, alisikika akiwatuhumu Wabunge hao wa CCM.
Taarifa zinaonesha kuwa Mbowe sasa ameukabidhi mpira wa kashfa hiyo kwa Tundu Lissu ambaye ameahidi kuucheza ipasavyo. Kwa kuanzia, Lissu amepanga kuandika waraka-wa-kutaka-ufafanuzi kwa Rais Magufuli kuhusu kashfa hiyo ikizingatiwa kuwa Serikali ya Rais Magufuli inapinga na kupambana na rushwa.
Tayari Lissu amekusanya nyaraka mbalimbali za kushadidia kashfa hiyo na anapanga mikakati ya kuishughulikia hatua kwa hatua. Kuhusu waranti wa kukamatwa kwake, Lissu menukuliwa akisema hayo ni mambo ya kimahakama na yanapaswa kushughulikiwa kimahakama.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA