Kamanda wa Polisi mkoa wa Dar es salaam Simon Sirro, amesema kama Mkuu
wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, ana wasiwasi na Jeshi la Polisi
katika operesheni ya kutokomeza matumizi ya Shisha, achukue hatua zaidi
kwa sababu yeye ni kiongozi wao na ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na
Usalama Mkoani Dar es salaam.
Akiongea kupitia kipindi cha Sun Rise cha Times Fm leo asubuhi, Sirro
amedai wao kama jeshi la Polisi wanafanya kazi kwa mujibu wa Sheria na
Operesheni ya kutokomeza Shisha jijini inaendelea kama kawaida kilicho
baki ni Mwanasheria mkuu wa Serikali kuandaa mashtaka kwa Watuhumiwa.
“Watu wamekamatwa ni wengi, kimsingi kazi inafanyika, sasa huo ni wasi
wasi kama wasi wasi basi unabaki kuwa wasi wasi, kikubwa niseme
tunafanya kazi kwa mujibu wa sheria na kanuni, yeye ni mwenyekiti wangu
wa kamati ya ulinzi na usalama kwa hiyo ninaamini kama ana wasiwasi na
chombo chake najua atakuja kutuita na kutuambia nini cha kufanya.
“Lakini kama ana wasi wasi Zaidi yeye ni kiongozi wetu atajua atachukua
hatua gani dhidi ya sisi, kwa hiyo namuachia mkuu wangu wa kazi yeye
ndio atajua nini cha kufanya”
Akitolea ufafanuzi kama alipatiwa taarifa juu ya watu 10 waliotaka kumpa
‘Mlungula’ Mkuu wa Mkoa ili kumziba ‘Mdomo’ kukemea matumizi ya kilevi
cha Shisha, Kamanda Siro alisema hawezi kulisemea lolote swala hilo na
amemtaka Mtangazaji wa Sun Rise Stanslaus Lambat amuulize Mh Makonda
taarifa aliipeleka wapi na si yeye.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA