TAARIFA KWA UMMA
Leo Ijumaa 18.11.2016 Baraza la madiwani wa Jiji la Arusha limekutana
katika kikao chake Maalum. Kikao kilikuwa na ajenda moja tu “Mikataba ya
upangaji wa maduka ya Halimashauri”.Baada ya mwenyekiti kufungua kikao
Hoja ilitolewa kuwa KATIBU TAWALA WA WILAYA sio mjumbe wa Baraza na kwa
kuwa ni baraza maalum atoke nje,hoja iliyoungwa mkono na wajumbe wengi
hivyo Mwenyekiti wa kikao kumtaka KATIBU TAWALA WILAYA Ndg Devid
Mwakiposa atoke nje,na yeye kuheshimu na kutoka nje kisha kikao
kiliendelea
Kikao kiliendelea kujadili maazimio moja moja kama ilivyopendekezwa na
Kamati ya fedha na Utawala.Azimio namba tatu lililohusu hatma ya
wapangaji walio ndani,wenye leseni na ambao wanaendelea na biashara
ilijadiliwa kwa muda mrefu,na wajumbe wengi waliafiki kuwa Wapangaji
wapewe mkataba wa mwaka mmoja utakaoisha Juni 30 mwaka 2017,kwa bei
iliyopo na mwaka wa fedha 2016/17 ukianza bei mpya na mikataba ya miaka
mitano itasainiwa,kwa kushirikisha wadau wote na kwa mujibu wa sheria
za nchi
Wakati mjadala ukiendelea Mkurugenzi wa Jiji Ndg Athumani Kihamia
aliingilia mjadala kinyume cha sheria na kutamka kuwa kamwe hatosaini
mikataba, na akaamuru watumishi wote watoke nje ya Kikao na hivyo
kuvuruga kikao na kikao kuvunjika
1.Mkurugenzi wa Jiji amekiuka sheria,kanuni na taratibu kwa kuvuruga na
kuvunja kikao ambacho kimeanza na kimefika ajenda(Hoja) ya tatu.
2.Mkurugenzi wa Jiji amekiuka sheria na kanuni kwa kutaka kikao kijadili
hoja ambayo ni kinyume cha sheria ya serikali za mitaa mamlaka za miji 8
ya mwaka 1982 “Hakuna shughuli yoyote itakayojadiliwa katika mkutano
maalum wa Halmashauri isipokuwa ile tu iliyoelezwa kwenye taarifa ya
kuitishwa kwa mkutano huo”.
Kutokana na matendo haya ya ukiukwaji wa taratibu kanuni na Sheria Mkurugenzi Baraza limeamua yafuatayo,
Kuwa Mkurugenzi wa Jiji Bwana Kihamia amevuruga kikao mwenyewe ambacho
ameshiriki tangu mwanzo wa maandalizi yake ambayo yamegharimu fedha
ambazo ni kodi za wananchi wa Arusha,hivyo BARAZA limeamua kuwa gharama
za Baraza maalum la Tarehe 18.11.2016 Mkurugenzi wa Jiji la Arusha
atazilipa yeye ndg Athuman Kihamia,hii ni kwa kuwa yeye ndg Athumani
Kihamia ndie aliyevuruga kikao kwa maslahi yake binafsi
Kuwa maamuzi ya Baraza yataendelea kubaki,na kuwa Wafanyabiashara
waliopo ndani na ambao ndio wenye leseni ndio wafanyabiashara Halali
Baraza linawataka wafanyabiashara wote Stend Ndogo,Soko la
Kilombero,Soko Kuu,Soko la Kijenge,Stend Kuu na maeneo mengine ya
biashara yanayomilikiwa na Halimashauri kuendelea kulipa kodi ya Pango
kwenye akaunti ya Halimashauri na kamwe si kwa MADALALI ambao kimsingi
hawatambuliki kisheria na wala hawana UHALALI wa kisheria,
Wapangaji wote waliomo ndani waendelee kutunza vyumba vya HALMASHAURI
hadi watakapopata maelekezo mengine kutoka Halimashauri(Baraza)
Baraza la madiwani linawaonya vikali MADALALI wa vyumba vya Halmashauri
na kuwa hawaruhusiwi kuwasumbua wapangaji,na hatua kali za kisheria
zitachukuliwa kwa yeyote atakayewasumbua wapangaji
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA