Mchakato wa katiba mpya mpaka sasa haueleweki hatima yake, na wala kwa sasa serikali ya awamu ya tano haina muda nayo. MAHENGA BLOG imeshtushwa.
Swali limeulizwa na mhariri wa TBC Tindo Mhando katika mahojiano ya moja kwa moja kati ya rais Mafugufuli na waandishi wa habari juu ya wapi katiba mpya imefikia mpaka sasa. Akijibu swali hilo, rais wa jamhuri ya muungano ya Tanzania amedai hakuwahi kuzungumzia katiba mpya kwenye kampeni zake pamoja na kuzunguka KM 46,500 kwa gari. 'una maswali ya kichokozi...sikuwahi kuzungumzia katiba mpya wakati wa kampeni zangu pamoja na kutembea km 46,500 kwa gari...niache kwanza niinyoshe hii nchi' amesema JPM.
Kupitia mahojiano haya yanayoendelea moja kwa moja kwenye ukumbi wa ikulu jiji Dar, imejidhihirisha kuwa, Tanzania kuipata katiba mpya bado haieleweki, hivyo kwa majibu hayo, tuendelee kufanya kazi zingine za maendeleo kuliko kuwaza katiba.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA