Katika kipindi cha mahojiano ya rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzani Dkt John Pombe Magufuli na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Ikulu jijini Dar, mwandishi wa habri toka BBC Sami Awami amemuuliza swali Mh. rais juu ya ukandamizaji wa siasa ambalo kidogo limempa 'stress'.
Sami aliuliza swali hilo kwa lugha ya kiingereza huku akianza kwanza kwa kumpongeza rais kwa maendeleo aliyoyafanya ndani ya muda mfupi, lakini swali lake lilikuwa ni juu ya wakosoaji wanaodai Mhe. rais anatumia maendeleo kukandamiza demokrasia, je hili analizungumziaje? '..critics say that you use development to supress democracy in the country, how do you argue on this?..' ameuliza Sami.
Swali hili lilionekana kama la kushitukiza, na katika kulijibu, Mhe. kidogo alipata kigugumizi, na baadaye ndipo akatumia ugomvi wa chama fulani waliokutana na kufukuzana wenyewe. '..demokrasia ipo, lakini ina mipaka...wapo chama fulani walikutana, wakafukuzana wenyewe, wakagombana wenyewe..' amesema JPM.
Aidha Dkt Magufuli ametumia ushindi wa vyama vya upinzani jijini Dar kwa umeya kuonesha uwepo wa demokrasia.
Sanjari na hayo, Dkt. Magufuli ameendelea kusisitiza kuwa, siasa zina wakati wake, siyo kila siku siasa kiasi cha kusahau shughuli za maendeleo.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA