Laydee amesema kauli aliyoitoa Mkurugenzi wa Vipindi wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba kuhusu kuwa tayari kucheza nyimbo zake akiwaruhusu, ni sahihi na ya kiutuzima.
Muimbaji huyo mkongwe ametoa kauli hiyo kwenye mahojiano na mtangazaji wa Nyemo FM, ya Dodoma, Winston Makangale.
“Nimeisikia kauli ya Ruge, kwa namna aliyoiongea na nafasi aliyokuwa nayo, sioni kama kuna kitu kibaya chochote alichokifanya kwa jinsi ambavyo amezungumza, naona amezungumza sahihi tu,” alisema.
Amesema yeye na Ruge hawajahi kuzungumza kwa miaka minne sasa.
“Hajanipigia simu na wala sijampigia simu, kwahiyo sio kwamba tumeongea kitu chochote lakini nayaona tu ni maamuzi ya kikubwa ambayo yamefanyika hapo. Hatujaongea kwasababu tulikuwa na mgogoro,” ameongeza
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA