Biblia ilivyookoa maisha ya mchezaji wa Chapecoense “Neto” kwenye ajali ya Ndege

<<<DOWNLOAD MAHENGA BLOG APP HAPA>>>




Wiki moja baada kutokea ajali mbaya ya ndege iliyokuwa na wachezaji wa timu ya Chapecoense inayoshiriki Ligi Kuu ya Brazil na kuua abiria 71 wakiwemo wachezaji wa timu hiyo, waandishi wa habari, makocha na wafanyakazi wa ndege hiyo, imetoka ripoti kuwa mchezaji Helio Neto aliyenusurika alikuwa akisoma Biblia kabla ya kutokea ajali.


Kwenye kipande kifupi cha Video kilichoonekana kwenye camera za ndege hiyo kimeonesha kuwa mchezaji huyo alikuwa akisoma Biblia muda mwingi akiwa kwenye ndege na hata baada ya ajali bado Biblia ilikutwa kwenye siti yake pamoja na yeye Neto kuwa kwenye hali mbaya.

Ukurasa ulioonekana kwenye Bibla ilikuwa ni kutoka kwenye kitabu cha Zaburi 63:6-8. Ambayo ina maneno haya;

“Wakati ninapokukumbuka kitandani mwangu, wakati wa makesha ya usiku natafakari juu yako. Kwa maana umenisaidia na katika kivuli cha mabawa yako napiga vigelegele kwa shangwe, nafsi yangu imekufuata karibu, mkono wako wa kuume unanishika sana.”

Baada ya kutokea ajali hiyo, Biblia ya mchezaji huyo ilikabidhiwa kwa mke wake ambaye alikiri wazi kuwa mume wake amekuwa mtu wa dini sana na huwa anatembea na Biblia yake popote anapokwenda.

Jumla ya watu 71 walipoteza maisha kwenye ajali ya ndege aina ya Avro RJ85 iliyotengenezwa nchini Uingereza baada ya kuanguka kwenye milima ya Medellin nchini Colombia, ambako timu ya Chapecoense ilikuwa inaenda kucheza fainali za Copa Sudamericana.

Chapisha Maoni

0 Maoni