Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Godwin Gondwe na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. William Makufwe, wakisalimia wananchi wa Kata ya Segera
Mhe. Godwin Gondwe akizungumza na wananchi wa Kata ya Segera Iliyopo Halamshauri ya Wilaya ya Handeni kwenye maadhimisho hayo
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni BW. William Makufwe akizungumza na wananchi wa Kata ya Segera kwenye maadhimisho hayo.
Mkuu wa TAKUKURU Wilaya Bi. Esta Mulima akizungumza na wananchi wa Kata ya Segera kwenye maadhimisho.
Mhe Diwani wa kata ya Segera Bw. Yassin Mtamike akifafanua jambo kwa wananchi wa Kata ya Segera.
Mkuu wa Wilaya akimpa kipaza sauti moja ya wananchi waliokua wakitoa kero za
Baadhi ya Maafisa wa TAKUKURU, Wilaya wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya.
Mkuu wa Wilaya akimuuliza jambo Mkuu wa TAKUKURU wilaya Bi. Esta MUlima juu ya utekelezaji wa maagizo yake
Baadhi ya wananchi wa kata ya Segera .
Mmoja ya wananchi waliokua wakitoa kero zao kwa Mkuu wa Wilaya
Wananchi Wilayani Handeni wametakiwa kufuata maadili katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku ili kujihahakikishia huduma bora za jamii.
Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe alipokuwa akisikiliza kero za wananchi wa Kata ya Segera iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Handeni jana katika maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za Binanadamu Kiwilaya yaliyoandaliwa na taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU).
Gondwe alisema “ Maadli ni imani njema, sehemu yoyote yenye maadili haki za binadamu hufuatwa, hakuna ardhi itakayouzwa kiholela, wagonjwa watatibiwa vizuri kwenye vituo vya afya, wageni wataingia kwenye maeneo yetu kwa kufuata taratibu za nchi na shughuli zote zitafanyika kwa misingi ya Haki”.
Aidha aliwataka watumishi wa umma na wananci kwa ujumla kufuata sheria, taratibu na kanuni pasipo kujali wala kubagua rangi au cheo cha mtu yeyote. Alisema kuwa Rushwa ni adui wa haki na kuwataka kuikataa kwa kauli na vitendo.
Wakati huohuo Mkuu wa Wilaya ya Handeni alivunja baraza la Ardhi la Kata kwa kulalamikiwa na wananchi kutotekeleza maajukumu yeke na kuwaagiza TAKUKURU Wilaya ya Handeni kulichunguza hadi ifikapo mwishoni mwa mwezi Januari 2017, na mapungufu yoyote yatakayobainika basi hatua za kisheria zichukue mkondo wake maramoja.
Vilevile aliwaaagiza Maafisa Watendaji wa Kata na Vijiji kusimamisha shughuli zote za kilimo zinazofanywa kwenye msitu wa hifadhi ya kijiji
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. William Makufwe aliwataka Maafisa Watendaji na wenyeviti wa Vijiji kusimamia miradi yote ya maendeleo kwa maadili na uadilifu kutokana na dhamana kubwa waliyonayo kwenye maeneo yao ya kiutawala. Vilevile aliwataka kusoma tarifa za mapato na matumizi na kuwa tayari kujibu hoja za wananchi kuhusu taarifa za mapato na matumizi. “Mtendaji atakayeshindwa kusoma taarifa za mapato na matumizi atakua amejiondoa mwenyewe kwenye nafasi yake” Alisema Makufwe.
Mkuu wa TAKUKURU Wilaya Bi. Esta Mulima, alisema TAKUKURU itaendelea kupambana na Rushwa kikamilifu na kuendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu madhara ya Rushwa. Aliwataka wananchi kufichua vitendo vya rushwa vinapotokea au dalili za vitendo hivyo ili hatua ziweze kuchukuliwa.
Maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za Binadamu hufanyika kila tarehe 10 Disemba Kitaifa, na Wilayani hapa yalifanyika tarehe 8 Disemba kutokana na Muingiliano wa Majukumu yakiongozwa na kauli mbiu isemayo.
“kujenga na kukuza maadili, haki za binadamu, uwajibikaji, utawala bora na Mapambano dhidi ya Rushwa”.
Alda Sadango
Afisa habari
Halmashauri ya Wilaya ya Handeni
9 Desemba 2016.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA