Wachimbaji hao wameikataa miamba taka hiyo mara baada ya kubaini kuwa hayana dhahabu bali yanafaa kwa ujenzi wa nyumba na kusema kuwa miamba hiyo siyo ambayo iliagizwa na Rais kutolewa kwa wananchi hao.
Wachimbaji hao wameongeza kuwa gharama ya kubeba mawe hayo mpaka kuyafanyia mchakato wa kupata dhahabu ni kubwa zaidi ya dhahabu itakayopatikana huku wakisema wamechelewa kutoa miamba taka hiyo ili kufanya uchakachuaji.
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga amesema kuwa sababu ya kuchelewesha kutoka kwa wakati miamba taka hiyo ni kutokana na agizo la Rais, masharti mengi yalikuwa yakihitajika kutekelezwa na serikali katika kuipata miambataka hiyo.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA