Maalim Seif: Prof. Lipumba, Jeshi la Polisi, Msajili wa Vyama Wanaihujumu CUF

KATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad amesema aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho, Prof. Ibrahim Lipumba, Jeshi la Polisi na Msajili wa Vyama vya Siasa wamekuwa wakishirikiana kufanya hujuma dhidi ya chama chao.

Maalim Seif ameyasema hayo leo wakati akiongea na wanahabari katika Ukumbi wa Mikutano wa Peacock Hotel jijini Dar es Salaam.
“Kama mnavyofahamu, Chama Cha Wananchi (CUF) kinapitia wakati mgumu kutokana na mambo yanayofanywa na msajili wa vyama pamoja na Lipumba. Lipumba na Jeshi la Polisi wamekuwa wakishirikiana kufanya hujuma dhidi yetu.

“Jeshi la Polisi limekua likivamia na kuvuruga mikutano halali ya chama cha CUF kwa kushirikiana na msajili wa vyama vya siasa. Prof. Lipumba akiwa na kundi lake la wahuni walivamia hoteli ya Blue Pearl na kuvuruga mkutano huku polisi wakishuhudia.

“Uongozi wa chama ulifungua kesi kituo cha Magomeni lakini mpaka sasa hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa na kumekuwa na matukio ya utekaji wa wanachama yanayofanywa na makundi ya Prof. Lipumba pamoja na kuripotiwa bado hakuna kilichofanywa.” Amesema Maalim Seif

Aidha Maalim Seif ameongeza kuwa;
“Mpaka muda huu gari lililokuwa polisi kama ushahidi limeondolewa na watuhumiwa wameachiwa huru na Jeshi la Polisi.
“Wafuasi wa Prof. Lipumba wamekuwa wakitoa vitisho kwa wanachama na viongozi huku wakidai jeshi la polisi ni sehemu yao.”

Yafuatayo ni mengine aliyoyatolea ufafanuzi Maalim Seif;

Maalim Seif: Makundi ya Prof. Lipumba yamekuwa yakivamia ofisi za chama na kuharibu mali pamoja na kuwapiga walinzi wakiwa na askari.

Maalim Seif: Wafuasi wa Prof. Lipumba wakiwa na askari walikwenda ofisi za chama Bagamoyo ambapo walivunja ofisi na kuharibu nyaraka za chama.

Maalim Seif: Msajili wa vyama vya siasa Jaji Mutungi amekua akitoa maelekezo ya kuvuruga mikutano ya CUF kwa kutumia jeshi la polisi.

Maalim Seif: Jaji Mutungi alimuandikia barua Prof. Lipumba na kuinakili kwa IGP ili watoe ulinzi wa jeshi la polisi wanapovuruga mikutano.

Maalim Seif: Jeshi la Polisi limempa kibali Prof. Lipumba kufanya mikutano maeneo mbalimbali ya nchi huku akiwa na ulinzi wa askari.

Maalim Seif: Wakati huo Jeshi la Polisi limezuia viongozi halali wa CUF kufanya mikutano sehemu yoyote nchini pamoja na kuwaweka ndani wabunge.

Maalim Seif: Pamoja na kutolewa taarifa za matukio yote ya utekaji na uharibifu unaofanywa na wafuasi wa Lipumba bado jeshi limekaa kimya.

Maalim Seif: Niliwaandikia barua Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara na Lindi kuwaomba kibali cha mkutano ili kufata sheria walitupa kibali.
Maalim Seif: Siku ya mkutano OCD wa mtwara alituma askari waliovuruga mkutano wangu na viongozi na waliwachukua wasaidizi wangu mpaka polisi.

Maalim Seif: Tulifanya mazungumzo na jeshi la polisi mtwara na wabunge wa CUF na wakasema wao hawana majibu na wamepata agizo kutoka juu.

Maalim Seif: Orodha ya matukio ya uhalifu kwa Chama Cha CUF kati ya Msajili wa Vyama, Jeshi la Polisi na Prof. Lipumba ni mengi sana.

Maalim Seif: Jeshi la Polisi nchini limekuwa likitumika kisiasa na kuungana na makundi ya wahalifu ili kutekeleza matakwa ya viongozi.

Maalim Seif: Wote tunafahamu Prof. Lipumba aliamua kujiuzulu mwenyewe pamoja na kushauriwa sana na viongozi wa chama na dini alikataa.

Maalim Seif: Prof. Lipumba alisema nafsi yake inamsuta kuendelea na vuguvugu la UKAWA wakati kuna mambo hajaafikiana nayo.

Maalim Seif: Pamoja na Prof. Lipumba kujiuzulu bado Chama kilifanikiwa kutetea na kuongeza majimbo ya ubunge kwenye uchaguzi mkuu.

Maalim Seif: Vyama vya Upinzani vilivyoungana UKAWA, viliingia kwenye uchaguzi mkuu vikiwa na mshkamano na kuweka upinzani mkubwa.

Maalim Seif: Mimi nilishinda uchaguzi mkuu Zanzibar lakini tume na serikali zilifuta matokeo ili kutaka kupotosha ukweli.

Maalim Seif: Chaajabu Prof. Lipumba amekuwa na urafiki mkubwa na viongozi wa serikali wakati alikuwa na tofauti nao ikiwemo Waziri Nape.

Maalim Seif: Mpaka leo hatuna barua wala taarifa ya sababu zilizomfanya Prof. Lipumba ajiuzulu nafasi yake na kutaka kurudi tena.

Maalim Seif: Kutokana na kuonesha msimamo dhidi ya dhuluma inayofanywa na Prof. Lipumba na serikali dhidi ya chama cha CUF, amezuia ruzuku.

Maalim Seif: CUF ina taratibu zake ikiwemo kuonywa kusimamishwa na kufukuzwa uanachama. Ingawa sio lazima hatua zote zipitiwe.

Maalim Seif: Kuanzia August 2016 Msajili wa vyama hajatoa ruzuku ya chama cha CUF kwa maelezo kuwa chama kina mgogoro wakati alitaka kumpa Lipumba.

Maalim Seif: Mimi kama katibu mkuu wa chama niko tayari kufanya mdahalo na Lipumba ingawa yeye alikimbia kikao na Mimi.

Chapisha Maoni

0 Maoni