Wasichana
wawili waliopatikana wakipigana busu katika paa la nyumba
wamewasilishwa mahakamani katika mji wa Marrakesh nchini Morocco
wakishtakiwa na tabia za wapenzi wa jinsia moja ,mmoja wa mawakili wao
waliambia AFP.
Wasichana hao wenye umri wa miaka 16 nad 17 mtawalia walishtakiwa kwa kushiriki tendo lililo kintume na maumbile yao.
Wawili hao walikamatwa mwezi uliopita baada ya kuripotiwa na familia zao.
Walipatikana wakikumbatiana na kupigana busu juu ya paa.
Wasichana hao wanakabiliwa na vifungo vya miezi sita hadi miaka mitatau jela.
Walikana yale yalioandikwa katika ripoti ya polisi kwamba walikuwa
wakifanya vitendo vya wapenzi wa jinsia moja na kusema kuwa uhusiano wao
ni wa kirafiki.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA