Na sasa baada ya kujiridhisha pasipo shaka yeyote kwamba Joseph L. Fuime
aliuza matokeo ya ushindi wake wa UBUNGE kupitia CHADEMA uchaguzi mkuu
2015 katika Jimbo la Songea Mjini sasa amefukuzwa UANACHAMA wa CHADEMA
Rasmi. Na sasa anachokifanya kuhakikisha anavuruga chama wilaya ya
Songea Mjini. Amewakusanya vijana na baadhi ya wafuasi wake kushinikiza
arudishwe kwenye chama. Jambo ambalo siyo sahihi na hata haya mambo
yanayorushwa na Bwana Andrea wa kata ya Mshangano kwa kujiita
mwanahabari ni kujaribu kufcha ukweli huu.
JINSI ALIVYOUZA USHINDI KWA LEONIDAS GAMA WA CCM
Taarifa kwa wapenda maendeleo na wote wasiojua ukweli kuhusu yalitokea
kuhusiana na matokeo ya uchaguzi mkuu wa ubunge jimbo la songea mjini
yaliyotangazwa siku ya jumatatu tarehe 26/10/2015.
Figisu za kushindwa uchaguzi au kuporwa ziliaza mapema sana kabla ya
kutangazwa kwa matokeo ambapo lilijitokeza kundi kubwa sana la wanaccm
wakiimba na kuashiria kwamba mgombea wao alikuwa ameshinda uchaguzi ule.
Lakini baadae ilijulikana kwamba mgombea wa chadema alikuwa ameshinda
uchaguzi ila kulikuwa na mbinu ya kuhakikisha anatangazwa aliyeshindwa
Leonidas Gama.
KUHUSU MGOMBEA WA CHADEMA NDUGU JOSEPH L. FUIME
Hakika mgombea wa chadema alishinda uchaguzi ule ila aliuza ushindi kwa
LEONIDAS GAMA ambaye ndiye mbunge wa Songea Mjini kwa sasa, na hii
inajidhihirisha kutokana ushahidi wa kimazingira na tofauti ya takwimu
za matokeo yaliyowasilishwa kwenye chama na timu ya kampeni ya Mgombea
wa chadema ndugu Joseph L. Fuime.
USHAHIDI WA KIMAZINGIRA
" Kutokuwepo kwa mgombea wa chadema Bwana Joseph Fuime kwenye kituo cha
majumuisho ya mwisho katika ofisi za manispaa, Kutokupatikana kupitia
mawasiliano ya simu kwa namba zake zote siku ya majumuisho,
" kutokukabidhi kwenye chama nakala halisi za matokeo ya kila kituo cha kupigia kura katika jimbo alilogombea yaani fomu Na. 21B
" Kufungua kesi bila kushirikisha chama, na hatimaye kesi kufutwa.
KUTOKUWEPO KWENYE KITUO
Kitendo cha yeye kama mgombea kutokuepo kwenye kituo cha majumuisho na
kumuacha wakala wake wa majumuisho ndugu JONAS KAWELELA aliyekuwa
mwanafunzi wa chuo kilichofutwa cha St. Joseph ilikuwa ni picha ya awali
na wazi inayodhihirisha ufedhuli wake alioufanya kwa wapigakura wa
jimbo la songea mjini.
Hata juhudi za kumtafuta ziligonga mwamba kwani kwa muda wote wa
majumuisho licha ya yeye kutokuwepo pia simu zake za mkononi kwa namba
zake zote hakupatikana mpaka ilipotimu saa 11 jioni ndipo alipatikana na
kusema kwamba alikuwa nyumbani licha ya kwamba viongozi na RB walikuwa
wakifika nyumbani na kuambiwa hayupo
KUTOKUKABIDHI NAKALA ZA MATOKEO
Hili nalo ni ushahidi wa kutosha kwamba aliuza ushindi, kwani baada ya
uchaguzi kilifanyika kikao cha tathmini katika ofisi za chama wilaya
ambapo kamati tendaji ya wilaya, timu ya kampeni na yeye mwenyewe Fuime
alikuwepo katika kikao hicho. Ambapo wakala wake bwana Kawelela
alithibitisha kwa chama pasipo shaka kwamba Fuime alishinda ubunge na
wangepabambana hadi tone la mwisho kuhakikisha wanapata shindi kwa
kwenda kufungua kesi mahakamani.
Naye Joseph Fuime hakukanusha jambo hilo, lakini baada ya maelezo ya
wakala kwa viongozi waliwataka timu ya kampeni kukutana na secretariati
ya chama wilaya wakiwa na nakala original za matokeo za kila kituo na
kujumlisha kwa pamoja ili kujiridhisha kama kweli tulihinda ili chama
kiweze kutoa taarifa kwenye ngazi za juu kwa ajili ya kupatiwa msaada wa
kisheria, kabla hata ya kufanyika hilo viongozi walishangazwa sana
kukuta taarifa zimezagaa mitaani kwamba Fuime J. Amefugua kesi mahamama
kuu!
Viongozi walipoona waliyoagiza hayakufanyiwa kazi waliamua kuwaita timu
ya kampeni ambayo ilikuwa na viongozi watano kutoka kamati tendaji ya
wilaya ya songea mjini na wengine toka chuo cha ST. Joseph Ruhuwiko
ambao walitokana na uteuzi wa mgombea mwenyewe ili kukamilisha idadi ya
watu kumi. Hawa hapa chini ni wajumbe waliotokana na chama:-
1. Rhoda Komba - m/kt wa BAWACHA wilaya
2. Seif A. Seif - m/kt Baraza la wazee wilaya
3. Milanzi - mjumbe wa kamati tendaji
4. Ajaba nditi - mjumbe wa kamati
5. Omary Hassan - alikuwa m/kt BAVICHA wilaya kabla ya kujiuzuru nafasi yake.
Nakuwaelekeza kwamba wanatakiwa kukabidhi nakala halisi za matokeo ili
majumuisho yafanyike ili chama kiweze kijiridhisha na hata kutoa hali
mbaya ambayo ilishajitokeza kwa wazi kwamba bwana Fuime ameuza.
Hilo halikufanyika kwani wajumbe wa timu walirudi na majibu mepesi
kwamba nakala alikwa nazo mgombea na kila walipomfuata hawakumkuta, hadi
pale katibu wa wilaya alipoandika barua kwa Bwana Fuime kumtaka
kukabidhi nyaraka hizo kwenye chama haraka iwezekanavyo, Hata hivyo
barua hiyo haikujibiwa. Hata hivyo chama kilimvumlia na kumtumia barua
nyingine ya kukumbusha barua ya awali nayo haikujibiwa. Baada ya ukimya
huo chama kiliingiwa na shaka kwamba pengime kulikuwa na mpango ovu
dhidi ya hizo nakala na kwamba kwa nini hataki kukabidhi kwenye chama?
Kiliitishwa kikao cha dharura cha kamati tendaji ambapo wajumbe
walikubaliana katibu kumwandikia barua ya kumtuhumu kwa mambo yafuatayo
baada ya kuonyesha darau kwa viongozi wa chama na chama:-
1. Kwa nini hakuwepo kwenye kituo cha majumuisho pale ofisi za manispaa
yalipokuwa yanafanyikia majumuhisho hayo licha ya sheria za uchaguzi
kumtambua kama wakala namba moja?
2. Ni kwanini hakujibu barua za chama zilizoandikwa kwake licha ya kuzipokea kwa dispatch?
3. kwa nini hataki kukabidhi nakala za matokeo (Fomu Na. 21B) ya uchaguzi mkuu wa 2015 za kila kituo cha uchaguzi?
4. kwa nini alifungua kesi ya uchaguzi bila kutoa taarifa rasmi ya
maandishi kwenye chama licha ya kushauriwa na chama kufanya hivyo kwenye
kikao cha tarehe 27/10/2015?
Baada ya barua hiyo hakuna kilichofanyika ndipo chama kilipofikia hatua
ya kumsimamisha uana chama wake hadi pale atakapojibu barua na kukabidhi
nakala zake.
Baada ya hatua hizo aliandika barua na kwenda hadi makao makuu na kutaka
kukata rufaa ambapo alipeleka barua yake hiyo makao makuu bila hata
kunakilisha kwa ngazi ya wilaya, mkoa na kanda.
Baada ya barua hiyo tarehe 13/4/2016 kilifanyika kikao kwa agizo
la katibu mkuu kwa uwakilishi wa Mkurugenzi wa organaizesheni na mafunzo
wa CHADEMA ndugu Kigaila Benson kilichokutanisha kamati tendaji ya
wilaya ya songea; bwana Fuime; na baraza la uongozi la mkoa.
Kikao kiliaza kwa kusomewa barua ambayo alipelekwa makao makuu ya chama
bila viongozi kufahamu. Kila hoja ilijibiwa ingawa kimsingi haikuwa ya
kukata rufaa bali ilikuwa ya majungu dhidi ya viongozi wake.
Aliulizwa na Kigaila kuhusu tuhuma alizopewa na chama wilaya kama ifuatavyo:-
1. Kuhusu kutokuwepo kwenye kituo cha majumuisho - alikiri kwamba ni
kweli hakuwepo, alipoulizwa kwanini hakuwepo? - alijibu ni kwasababu
alishajua matokeo ya kwamba ameshindwa baada ya kujumlisha matokeo ya
vituo vyote kwa kushirikiana na timu yake ya kampeni usiku wa saa 7 wa
kuamkia siku ya jumatatu tarehe 26/10/2015 hivyo hakuona umuhimu wa
kuwepo kwenye kituo. ikiwa ni tofauti na maelezo yaliyotolewa na meneja
kampeni wake kwenye kikao cha tarehe 27/10/2015 kwamba bwana Fuime
alishinda ila ameporwa ushindi na wangetumia hadi tone la mwisho la damu
yao katika kudai haki yake na siku hiyo hakukanusha ikiwa naye
alikuwemo kwenye kikao.
Na alipoulizwa ikiwa aliutaarifu uongozi juu matokeo ya huo usiku? - alikiri
hapana. ila alitegemea wale wajumbe wa kamati ya kampeni wangalisema
kwenye chama, ili viongozi waweze kuwajulisha wanachama na pengine hata
wasingeumizwa kwa kupigwa na mabomu kama ilivyotokea siku ya jumatatu
ile. Alipoulizwa baada ya yeye na timu ya kampeni kujumlisha
walipata matokeo yapi? - alijibu ni yale yaliyotangazwa na mtangaza matokeo pale manispaa.
Aliulizwa hayo matokeo walijumlishia wapi? - alijibu walijumlishia
nyumbani kwake, aliulizwa kwanini walijumlishia nyumbani kwake na siyo
ofisini? - alijibu kwamba awali muongozo wa chama uliwataka kuandaa
ngome ambapo shughuli zote za uchaguzi na kampeni zingefanyikia hapo, na
kwamba ngome ilipatikana lakini hawakuweza kumudu gharama, hivyo
aliamua kuweka ngome nyumbani kwake.
Aliulizwa Je alitoa taarifa kwenye chama kwamba ameamua kuweka ngome nyumbani kwake ili wamshauri? - alijibu hapana hakutoa taarifa kwa viongozi wa chama. Aliulizwa kwa nini? Alikaa kimya kuashiria hakuwa na majibu ya swali lile.
2. kuhusu kutojibu barua - alikiri kupokea barua zote ila hakutaka
kuzijibu ila alitaka aitwe, jambo ambalo lilitafsiriwa ilikuwa ni dharau
ya dhahiri kwa uongozi wake halali wa wilaya.
3. Kuhusu Kutokabidhi nakala - alikiri kwamba ni kweli ila alisema
kwamba zilikuwa mahakamani zilipelekwa kama EXBIT. lakini ikumbukwe kesi
ilifutwa kabla ya kuaza hatua ya kusikiliza na hayo yanathibitishwa na
nakala ya ufunguaji wa kesi ya mahakama kuu ambayo haina mahali ambapo
inaonesha kwamba nakala ziliwasilishwa mahakama kuu Pale mkoa wa Ruvuma.
4. Kuhusu kufungua kesi bila taarifa rasmi kwenye chama - alisema
yeye alijua kwamba kwa namna iliongelewa kwenye kikao cha tarehe
27/10/2015 ilitosha na hakuwa na sababu ya kupeleka taarifa rasmi tena
kwa maandishi kwenye chama. Alipoulizwa ikiwa ilikuwa muhimu kujulisha
chama kuhusu kesi kwa barua? - alijibu haikuwa na umuhimu.
MAELEZO YAKE MENGINE BINAFSI (nyongeza)
Alisema kwamba watu wanamtuhumu kwamba amechukua hela mil. 300, na
kwamba milion mia tatu (mil. 300) ni fedha nyingi sana watu wasiongee
ongee hivyo. [hapa kuna walakini maana hakubisha kwamba hakuchukua ila
alisema kwamba hiyo mil. 300 ni nyingi sana kumbe inawezekana alichukua
lakini siyo kiasi hiko]
MAAZIMIO YA KIKAO YALIYOTOLEWA NA NDG. KIGAILA MKURUGENZI WA OGANAIZESHEN NA MAFUNZO TAIFA
Baada ya kikao kile maazimio yalikuwa ni kwamba bwana Fuime anatakiwa
kujibu barua zote alizoandikiwa na chama; kukabidhi nakala za Fomu Na.
21B kwenye chama ndani ya siku 14, tangu tarehe ya kikao.
UTEKELEZAJI WA MAAZIO NA NDUGU JOSEPH L. FUIME
Baada ya kikao kile hakuna hatua za makusudi zilichuliwa na mhusika kwa
siku 14 alizokuwa amepewa na ndg Kigaila bali alikabidhi photocopy za
nakala na siyo nakala orijina Fomu Na. 21 kuptia kwa mzee Mwasote na
Bwana Octavian tarehe 28/06/2016 ikiwa ni karibu miezi miwili.
Mara baada ya kupokelewa zile copy za nakala uongozi wa wilaya kupitia
kwa secretariati yake walipitia nakala moja baada ya nyingine na
kuzijumlisha ambapo majibu yake ilikuwa ni
" Waliopiga kura walikuwa 77,554
" Zilizoharibika 1,220
" Mgombea wa chadema 40,786
" Mgombea ACT-Wazalendo 436
" mgombea wa CCM --
ukichukua (77,554 - 40,786 =36,768 ); (36,768 - 436 = 36,332 ); (36,332 -
1,220 = 35,112); hii maana yake ni kwamba figure ya mwisho ya 35,112
ndizo kura alizopata mgombea wa CCM ambapo kwa jibu jepesi lisilohitaji
kwenda shule ni kwamba Mgombea wa Ubunge wa CHADEMA JOSEPH L. FUIME
alishinda uchaguzi ule ila aliuza.
Matokeo haya kupitia kwenye nakala yalitofautiana yale yaliyowasilishwa
na timu ya mgombea ambayo yalikuwa ni yale yaliyotangzwa na msimamizi wa
uchaguzi wa manispaa (mkurugenzi), ambapo hili timu ya kampeni ilikili
katika repoti yao kwamba walilazimika kuchukua matokeo yale kwa kuwa
mgombea alikatalia kutoa nakala, ila hili jambo hawakueleza kwenye
ripoti na ndo maana walichukuliwa hatua kuhusika kuhujumu uchaguzi ule.
HATUA ZILIZOCHUKULIWA NA UONGOZI DHIDI YAKE
Na sasa baada ya kujiridhisha pasipo shaka yeyote kwamba Joseph L. Fuime
aliuza matokeo ya ushindi wake wa UBUNGE kupitia CHADEMA uchaguzi mkuu
2015 katika Jimbo la Songea Mjini sasa amefukuzwa UANACHAMA wa CHADEMA
Rasmi. Na sasa anachokifanya kuhakikisha anavuruga chama wilaya ya
Songea Mjini. Amewakusanya vijana na baadhi ya wafuasi wake kushinikiza
arudishwe kwenye chama. Jambo ambalo siyo sahihi na hata haya mambo
yanayorushwa na Bwana Andrea wa kata ya Mshangano kwa kujiita
mwanahabari ni kujaribu kufcha ukweli huu.
Ushauri wetu sisi wapenda mabadiliko ni kwamba kuna kila sababu
kuwaeleza akina Halifa, Rhoda, Mustafa, Haule, Zamaradi wajue wanafanya
kazi ya Mtu na siku ukweli huu ukijulikana watakuwa wapoteza sifa kubwa
sana kwa usaliti wanaoufanya dhidi ya wapigakura wa Songea Mjini ambao
walimpigia kura nyingi sana Fuime akawauza.
Tumependa kuanika mambo haya ili wakubwa wajue maana kinachoonekana ni
kama viongozi wanalaumiwa lakini ukweli ndo huo hatuwezi kuona chama
kinavurugwa na mtu mmoja anayejiita ana wafuasi wengi huku akijua kwamba
aliuuza matokeo ya uchaguzi ule.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA