DAR ES SALAAM: Gumzo kubwa ndani ya wiki iliyopita ilikuwa ni kuhusu msanii wa filamu Bongo, Wema Sepetu kujiweka kwa modo aliyefahamika kwa jina la Ibrahim Mgimbu ‘Calisah’ lakini siku chache baadaye Kajala Masanja akamjibu baada ya kudaiwa kujiweka kwa msanii wa filamu anayefahamika kwa jina la Mutra.
Habari za Kajala kujiweka kwa Mutra zilivujishwa na mtu wa karibu wa mastaa hao aliyeomba hifadhi ya jina lake huku ikidaiwa kuwa wamekuwa wakiongozana sehemu mbalimbali.
“Penzi la Kajala na Mutra ndiyo habari ya mjini, wanatoka kwa siri lakini ukikaa nao karibu utajua tu kuwa wana uhusiano, fuatilieni mtaujua ukweli,” alidai mtoa habari huyo.
Baada ya habari hizi kulifikia Ijumaa, Mutra alitafutwa kupitia namba yake ya simu ambapo alipopatikana alisema: “Mh! Ni kweli ila hatupendi kuweka wazi, lakini angeulizwa yeye kwanza, hata hivyo nipigie baadae nitakujibu vizuri kwa sababu nipo lokesheni.”
Alipopigiwa baadaye alisema kuwa Kajala ni mtu wake wa karibu wanafanya kazi zao za filamu. Alipobanwa kuhusiana na awali kukiri, alisema:“Dah! Naomba nisamehe kwa kukujibu hivyo, nilikuwa lokesheni ndiyo maana nikateleza kukujibu vile.”
Baada ya Mutra, Ijumaa lilimsaka Kajala kwa kumtumia ujumbe wa WhatsApp ambapo mahojiano kwa ufupi yalikuwa hivi:
Ijumaa: Kajala mambo, unadaiwa kutoka kimapenzi na msanii mwenzako Mutra, mnadaiwa kuwa karibu muda wote na mara ya mwisho mlionekana pamoja kwenye sherehe ya Steve Nyerere.
Kajala: Ndio hivyo.
Ijumaa: Ndio hivyo ni shemeji kwa sasa au? Funguka basi?
Kajala: Kimyaa.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA