Aliyewahi kuwa rais wa Cuba na mwanamapinduzi wa kijamaa Fidel Castro amefariki dunia leo tarehe 26.
Akiongea na televisheni ya taifa nchini humo, kaka yake ambaye pia ni rais wa sasa wa Cuba, Bw. Raul Castro amethibitisha taarifa hizo ambapo amenukuliwa akisema, "amiri jeshi mkuu wa Serikali ya mapinduzi ya Cuba amefariki leo hii tarehe 26 saa 22:46"
Mwanamapinduzi huyo aliyewahi kumpindua Batista Fulgence mwaka 1958 kwa ushirikiano wa karibu na aliyekuwa swahiba wake El Che Guevara amefariki akiwa na miaka 90.
MTOTO WA MKULIMA ALIYEJITABIRIA UMAUTI
- Fidel Castro alizaliwa nje ya ndoa (out of wedlock) mnamo mwaka 1926 na baba yake aliyekua mkulima wa MIWA na mama yale alikua 'MTUMISHI WA NDANI' nyumbani kwa baba yake
- Ni Baba wa Mtoto Mmoja tu Fidelito (little Fidel).
- Aprili 13 mwaka huu alitimiza miaka 90.
- Ndoa yake ilivunjika mara tu baada ya kutoka kifungoni, japo mkkewe aliomba talaka tangu Castro akiwa kifungoni
- Castro aliiibuka Mwanasheria Nguli (University of Havana) na Mwanamapinduzi wa Karne Nyingi ambaye alikamatwa baada ya jaribio la kuiangusha serikali ya Fulgencio Batista's na kuhukumiwa jela miaka 15 kifungo kilichompa umaarufu sana
- Aliyebobea kwa Sigara Kali hadi mwaka 1985 (Chain Smoker)
- Aliamua Kufuga Midevu ili aokoe muda wa kunyoa (If you calculate 15 minutes a day to shave, that is 5,000 minutes a year spent shaving,")
- Ameishi akitambulika kama Dikteta wa miaka mingi na amekwepa zaidi ya majaribio 600 ya kutaka kumuua yakifanywa na CIA(Castro survived more than 600 assassination plots by the Central Intelligence Agency)
- Hotuba yale ya mwisho aliitoa April 19 mwaka huu akiwaaga wanachama wa chama cha Kikomunisti na kuwaambia kwamba ingawa yeye atatoweka duniani lakini Mapinduzi yataishi daima
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA