TANZIA: Aliyekuwa Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Zanzibar Jaji Maulidi amefariki dunia

Habari za kuaminika tulizozipa hivi punde ni kwamba Mh Jaji Zubeir Maulid alikuwa ni mwalimu na aliwahi kuwa Jaji na amewahi kushika nyadhifa mbalimbali Serikalini.

Jaji Zuberi pia amewahi kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar(ZEC).

Marehemu amefariki nyumbani kwake kwa mchina mjini Zanzibar na maziko yanatarajiwa kufanyika kwao Mbuzini Unguja.
 

Chapisha Maoni

0 Maoni