Hospitali ya Taifa ya Muhimbili imesema kuwa aliyewahi kuwa Waziri wa
Elimu, Mhe. Joseph Mungai ambaye amefariki dunia leo, hajafia katika
hospitali hiyo.
Msemaji wa Hospitali hiyo,
Aminiel Eligaesha amesema kuwa marehemu Mungai amefikishwa katika
hospitali hiyo akiwa tayari amekwisha fariki na kwamba kwa upande wao
hawajatoa matibabu yoyote zaidi ya huduma ya chumba cha kuhifadhia maiti
(Mochwari)
"Ni kweli tumempokea Mungai, lakini alikuwa tayari amekwisha fariki,
tunachosaidia sisi ni mochwari tu, kwahiyo kusema kuwa amefia Muhimbili
siyo sahihi" Amesema Eligaesha.
Kuhusu chanzo cha kifo chake, Eligaesha amesema hadi sasa bado
hakijafahamika, hadi uchunguzi utakapofanyika kwa kuwa hakufia katika
hospitali hiyo. "Hatuwezi kusema nini chanzo hilo ni jukumu la familia,
na pia kwa kuwa hajafia hapa hatuwezi kujua hadi postmoterm ifanyike,
kwa sasa amehifadhiwa hapa" Alimalizia Eligaisha.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA