Katibu
Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini Kenya (COTU), Bw.
Francis Atwoli amesema anaikubalia kasi ya Rais Magufuli katika
kupambana na rushwa.
Pia amewataka Watanzania wamuunge mkono badala ya kulalamikia kasi kwani
wao wanatamani mwakani aende kugombea kwao katika uchaguzi mkuu ujao.
Ametoa kauli hiyo katika Mkutano Mkuu wa Sita wa Shirikisho la Vyama
vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) katika ukumbi wa Mwalimu Julius K.
Nyerere ulioko Chuo cha Mipango, nje kidogo ya mji wa Dodoma,
uliofunguliwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
Ninawasihi wanaTUCTA suala la rushwa msilipe nafasi. Mpambane nayo kwa
sababu kule kwetu imeota mizizi. Muungeni mkono Rais Magufuli, badala ya
kulalamika kuwa kasi yake ni kubwa mno. Mnasema eti ana spidi sana,
mkiona taabu mtuazime japo kwa mwaka mmoja ili aje atunyooshee mambo
kule kwetu,” alisema huku akishangiliwa.
Amewataka wahimize uhusiano uliopo baina ya vyama vya wafanyakazi,
waajiri na Serikali iliyopo madarakani na kuwataka wadumishe umoja
miongoni mwa viongozi na wanachama mara baada ya kumalizika kwa
uchaguzi.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA