Wanafunzi wa shule ya Academic International school, Harshvardhan Kabla (kushoto) ambaye ameshika nafasi ya kwanza duniani katika somo la Kompyuta kwa wanafunzi wa “A Level” kwa mitihani ya Cambridge na Abishek Sankaranarayanan(kulia) ambaye ameshinda nafasi ya kwanza kwa somo la hisabati kwa mitihani ya Cambridge kwa wanafunzi wa kidato cha nne wakiwa katika picha ya pamoja katika sherehe maalum ya kuwapongeza.
Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni wa India, Inder Jit Sagar akimkabidhi cheti na kombe mwanafunzi wa Shule ya Academic International, Harshvardhan Kabla (kulia) kwa kushinda nafasi ya kwanza duniani katika somo la Kompyuta kwa wanafunzi wa “A Level” kwa shule zinazofuata mtahala wa Cambridge.
Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni wa India, Inder Jit Sagar akimkabidhi cheti na kombe mwanafunzi wa Shule ya Academic International, Abishek Sankaranarayanan(kulia) kwa kushinda nafasi ya kwanza duniani katika somo la Hisabati kwa wanafunzi wa “O Level” kwa shule zinazofuata mtahala wa Cambridge.
Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni wa India, Inder Jit Sagar (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na walimu wawili wa shule ya Academic International, Walter Mlowe ambaye anafundisha somo la Hisabati na Thadei Mwinuka ambaye anafundisha somo la kompyuta. Walimu hao walitunukiwa vyeti kwa kazi nzuri ya ufundishaji.
Mkurugenzi wa shule ya Academic International, Yusuf Kalindaga akizungumza katika hafla maalum ya kuwapongeza wanafunzi , walimu na wafanyakazi wa shule hiyo kwa kufanya vyema katika mitihani ya Cambridge.
Mkuu wa shule ya ya Academic International, Shyama Santhosh ( wa kwanza kushoto) akisema jambo katika sherehe hiyo ya kuwapongeza wanafunzi hao na walimu.
Baadhi ya wazazi na wanafunzi wa shule ya Academic International wakiwa katika hafla hiyo
Wanafunzi wawili wa shule ya Academic International ya Tanzania wameweka historia katika mitihani ya mtahala wa Cambridge baada ya kushinda nafasi ya kwanza duniani katika masomo ya hisabati na kompyuta.
Wanafunzi hao ni Harshvardhan Babla aliyekuwa wa kwanza katika mtihani wa somo la kompyuta kwa wanafunzi wa kidato cha tano Abishek Sankaranarayanan aliyeshinda nafasi ya kwanza katika mtihani wa hisabati kwa wanafunzi wa kidato cha nne.
Wanafunzi hao walikabidhiwa vikombe na vyeti na mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni wa India, Inder Jit Sagar. Pia walimu wa masomo hayo, Thadei Mwinuka ambaye anafundisha somo la kompyuta na Walter Mlowe wa somo la hisabati nao walikabidhiwa vyeti vya pongezi kwa kufanya vizuri.
Akizungumza katika halfa maalum ya kuwapongeza wanafunzi hao na walimu wa masomo hayo, Mkuu wa shule hiyo, Shyama Santhosh alisema kuwa wamefarijika na ushindi huo ambao umeiletea sifa shule, walimu nan chi kwa ujumla.
“Huu ni ushindi mkubwa kwa shule, walimu nan chi kwa ujumla, mtihani wa Cambridge unafanywa na maelfu ya shule duniani na shule yetu imeibuka katika nafasi ya kwanza kwa masomo hayo mawili, ni jambo la kujivunia sana, hii inaonyesha kuwa walimu wetu wapo makini katika kufundisha,” alisema Santhosh.
Mkurugenzi wa shule hiyo, Yusuf Kalindaga amesema kuwa wanajivunia kwa matokeo hao mazuri ambayo yamewafanya kuwa shule pekee Tanzania kushika nafasi hizo za kwanza.
“Nimefarijika na kuvutiwa sana na matokeo ya wanafunzi hawa wawili, walimu wetu, Mwinuka ambaye anafundisha somo la kompyuta na Mlowe wa somo la hisabati kwa kufanya kazi kubwa kuhakikisha kuwa wanafunzi wanaowafundisha wanashika mafundisho yao na shule kwa sasa inafarijika kwa matokeo mazuri.
Akizungumza katika hafla hiyo Harshvardhan Babla aliyekuwa wa kwanza katika mtihani wa somo la kompyuta aliwapongeza walimu na viongozi wengine wa shule hiyo kwa mafundisho mazuri na kushika nafasi ya kwanza Duniani.
Babla alisema kuwa haikuwa kazi rahisi kwa mitihani ilikuwa migumu sana, lakini alizingatia mafunzo na kujibu vizuri maswali na kuibuka katika nafasi ya kwanza. Abishek Sankaranarayanan aliyeshinda nafasi ya kwanza katika mtihani wa hisabati alisema kuwa ushindi huo si faraja kwake tu, bali kwa wanafunzi wote wa shule hiyo, walimu na wafanyakazi wengine.
Abishek alisema kuwa amejituma kwa lengo la kushinda na bado anaaamini kuwa atafanya vyema katika mitihani mengine.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA